Friday, November 9, 2018
Leo ni kumbukumbu ya harusi ya Milton Obote na Maria Kalule
Friday, March 30, 2018
Jinsi ya kutamka kwa usahihi
Siku hizi siyo lazima kujifunza lugha ili kuweza kutamka vyema majina na maneno yanayotokana na lugha za kigeni.
Ukibofya kwenye alama hiyo utasikia matamshi sahihi ya neno husika.
Friday, March 23, 2018
Ukitaka kula usiende jikoni
Nina desturi ya kununua mahindi ya kuchoma yanayouzwa mitaani. Nilichoshuhudia miezi kadhaa iliyopita kimenipunguzia hamu ya kula tena mahindi hayo.
Nilisogelea mchoma mahindi na kuchagua mhindi uliyokuwa tayari juu ya jiko la mkaa. Baadaye kidogo, mmoja wa mahindi aliyokuwa akichoma ulianguka chini na kuseleleka mbali na alipokaa.
Alimtuma mwanae kuuokota chini na akaurudisha jikoni kuendelea kuuchoma baada ya kuufuta mchanga. Haukuwa ule mhindi niliyouchagua mimi ila nilitambua kuwa muda si mrefu atafika mteja kama mimi na kulishwa mhindi huo na, bila shaka, kuambukizwa minyoo.
Lakini haikuwa hatari ya kupata minyoo tu. Mchoma mahindi alikuwa na kikohozi. Na kila alipokohoa aliziba mdomo akitumia mkono wake wa kulia, ikiwa ni tabia ile ambayo baadhi wamefundishwa ili kuwakinga wengine kuathirika na athari za maambukizo yanayoweza kusambazwa na anayekohoa.
Tatizo ni kuwa ni mkono huo huo aliutumia kugeuzia mahindi aliyokuwa anachomea wateja, pamoja na langu. Mkono ulikuwa unatoka mdomoni na kushika mhindi.
Aliponiambia mhindi wangu umeiva, badala ya kuanza kula pale pale kama ilivyokuwa desturi yangu, nikamuomba aufunge vizuri nikaondoka nao lakini sikuula na ndiyo ikawa mwisho wa kununua mahindi ya njiani.
Labda kwa sababu nimeanza kulima mahindi nitakuwa nachoma mahindi ninayovuna shambani kwangu.
Nimewahi kusikia msemo kuwa ukitaka kula chakula cha mgahawa usiingie jikoni. Utakayoyaona huko yatakatisha njaa yako.
Friday, March 9, 2018
Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 una hitilafu kubwa
Friday, March 2, 2018
Hii ndiyo mila ya Kizananki ya kurudisha mahari
Nilichelewa kidogo kufika kwenye msiba na aliendelea kunipigia simu mara kwa mara kunihimiza nifike mapema kwenye msiba. Alisema: "huu ni msiba wenu, njoo haraka!"
Sikuelewa maana ya ule kuwa "msiba wetu" mpaka baadaye.
Katika mila ambayo ilifuatwa miongoni mwa Wazanaki, mume anaweza kurudishiwa mahari na ndugu wa mke ili kuhalalisha wanandoa wawili kuachana na mke kurudi kwa ndugu zake.
Hili hutokea kwa sababu za kutoelewana kwa wanandoa, na hasa kama ndugu wa mke wanaamini kuwa dada yao anateswa au kudhalilishwa na mume wake.
Nilichojifunza kwenye msiba ni kuwa Mwalimu Nyerere alirudisha mahari kwa mume wa shangazi yangu na shangazi akarudi kuishi miongoni mwa ndugu zake.
Kwa desturi ya enzi hizo mke anayerudi nyumbani anatunzwa na ndugu zake. Kwa huyo shangazi, Mwalimu Nyerere alimjengea nyumba na aliendelea kuishi kwenye kijiji cha Butiama mpaka alipofariki.
Kwa mila hii mahitaji yake yote makubwa pamoja na ya watoto wake yatatimizwa na ndugu zake. Aidha, inapotokea binti zake kuolewa basi mahari yao inachukuliwa na hao waliomrudisha nyumbani. Kwa mantiki hiyo, hata unapotokea msiba gharama za msiba zinabebwa na waliomtoa kwa mume wake.
Na ndiyo hapo nikaelewa kauli ya baba yangu mdogo: "huu ni msiba wenu!" Mwalimu Nyerere ana warithi wake ambao wanapaswa kurithi pia majukumu yake.
Lakini mila na desturi zinabadilika. Wakati wa msiba uliibuka ubishi mkali kati ya wazee juu ya mila hiyo. Baadhi yao waliona kuwa haipaswi kufuatwa kwa sasa.