Ngowi alichaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho la IBF/USBA uliomalizika Hilton Hawaiian Village Resort, jijini Honolulu, Hawaii, Marekani tarehe 2 Juni. Uteuzi wa Ngowi unafuatia juhudi zake alizozifanya kuendeleza shirikisho hilo katika bara la Afrika tangu ateuliwe na Rais wa zamani wa IBF/USBA Robert Lee Sr. mwaka 1999 jijini New Jersey, Marekani. Onesmo Ngowi anakuwa mtu wa kwanza kutoka bara la Afrika kushika nyadhifa kubwa katika taasisi ya ngumi duniani na hii inaisaidia sana Tanzania na bara zima la Afrika kijitangaza vyema katika nyanja mbalimbali kama vile utalii na bishara.
Katika
Kamati hiyo ya maandalizi kuna wajumbe sita nao ni ; Louis
Priluker wa Marekani, Roberto Rea wa Italia, Lahcen Oumghar wa
Uholanzi na Roberto Ramirez wa Mexico. Kamati hiyo itafanya shughuli zake
katika kipindi cha mwaka mmoja na itakutana mara nne kwa mwaka. Sekretarieti ya
Kamati ya Ngowi itakuwa katika jiji la New Jersey nchini Marekani kuliko na
makao makuu ya shirikisho hilo duniani.
Mkutano huo wa Honolulu uliazimia kufanya mkutano wa IBF
kwaka 2014 katika bara la Asia na mwaka 2015 IBF itafanya mkutano wake katika
bara la Afrika mahali ambapo patateuliwa.
Ngowi
anawahimiza Watanzania ambao wako katika uandaaji wa mikutano kuchangamkia
nafasi hii ambayo itawaleta watalii zaidi ya 1,000 nchini toka nchi zaidi ya 200
duniani. Hii ni nafasi ya nadra sana katika biashara na watanzania ni muhimu
wakachangamka kama wenzao wengine katika nchi zinazokuwa wenyeji wa mikutano
kama hii.
No comments:
Post a Comment