Alinijia Mzanaki mmoja mwaka 1961, mara tu baada ya kupata uhuru. Anataka kazi; anasema, "Mzanaki ndiye Rais, basi sisi Wazanaki tutainuka." Nikamwambia, "Nenda, uko utaratibu wa kupata kazi." Akaniambia, "Na mimi vilevile niende huko?" Nikamwambia, "Kwa nini usiende huko?" Akasema, lazima nije kwako; sasa Mwalimu wewe umekwisha pata, ndugu zako wengine vile vile wapate. Sasa tusipoanza sisi Wazanaki waanze nani? Na wakubwa ndio wa kula, na wakati wa kula umefika; basi tule!"
(Uk. wa 40)
Yameharibika mengi kwenye nchi hii kwa sababu viongozi wengi wanaamini kuwa uongozi ni sehemu ya kujineemisha wao na familia zao. Na kwa wale ambao hawana ndugu au marafiki kwenye sehemu muhimu za uongozi, uwezekano wa kupata ajira au haupo kabisa au ni finyu sana.
Mwalimu Nyerere |
1 comment:
Ndiyo maana wengine, pamoja na kuwa wanachama wa chadema, tumesema lowasa hafai kuwa kiongozi wa taifa hili. Send this word to vincent nyerere who is your brother and the chadema mara chairperson.
Post a Comment