Nimejihusisha na kazi ya kutangaza historia na utamaduni wa eneo la Butiama kwa zaidi ya miaka saba sasa, na natambua ni jinsi gani utamaduni wa eneo unavyoweza kuathirika unapotokea muingiliano wa haraka kati ya maeneo ya mijini na ya vijijini. Mawasiliano mazuri kati ya miji na vijiji yanaweza kuongeza kasi hiyo, na hali kadhalika, uamuzi wa kuanzisha wilaya mpya pia unaweza kuleta matokeo hayo hayo.
Wilaya mpya inakuja na ongezeko kubwa la wafanyakazi kutoka maeneo mbalimbali. Nao siyo kama wanakuja na tamaduni zao za asili tu, ila wanaleta zaidi tamaduni za miji, na hata sheria za miji. Matokeo yake ni kudumazwa kwa tamaduni za asili za maeneo hayo mapya ya wilaya, na hasa kama yalikuwa maeneo ya vijijini.
Mojawapo ya sehemu za burudani na starehe za Butiama zilizoibuka baada ya kuanzishwa kwa wilaya mpya ya Butiama. |
Msimamo wangu haulengi kutetea suala la ukabila, bali unalenga kulinda na kutunza mila na desturi za eneo mahususi kwa madhumuni ya kuendeleza utalii wa utamaduni.
No comments:
Post a Comment