Ni dhahiri kuwa matarajio ya mashabiki wengi wa soka Ulimwenguni, hususani juu ya matokeo ya baadhi ya mechi za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Afrika Kusini sasa hivi, hayajatimia.
Niliweka swali kwenye wavuti hii: "Timu ipi itashinda Kombe la Dunia?" Na ingawa majibu ni machache, yanaakisi yaliyokuwa matarajio ya wengi wanaofuatilia Kombe la Dunia.
Kati ya wasomaji watano wa wavuti hii, wawili walitabiri ushindi kwa Argentina, mmoja kwa Brazil, mmoja kwa Uingereza, na mmoja kwa Hispania. Timu zote hizo nne zimeshafungishwa virago kurudi makwao baada ya kufungwa na timu nyingine zinazoshiriki mashindano ya Kombe la Dunia. Timu ambazo washabiki wengi hawakuzifikiria zimebaki kwenye mashindano. Leo hii, wakati Ujerumani ikijiandaa kupambana na Hispania, ni Uholanzi peke yake iliyopata nafasi ya kuingia kwenye fainali ikisubiri mshindi wa pambano la leo.
Hoja yangu ya leo ni kuwa: utabiri wa nani anaweza kushinda mashindano ya Kombe la Dunia ni jambo gumu sana. Maradona na Argentina walikuwa wanatisha, na Brazil walipoisambaratisha Taifa Stars, tusiokuwa na uzoefu wa soka tuliamini kuwa ndugu zake Marcio Maximo wanaelekea kwenye kutwaa taji.
Lakini, kama ambavyo wataalamu wanasema, matokeo ni baada ya dakika tisini (au mia ishirini, pamoja na penalti).
Nikiulizwa sasa hivi, naitabiria Ujerumani ushindi baada ya kuona ilivyoiadabisha Argentina kwa 4-0. Nimeangalia kumbukumbu niliyonukuu miaka minne iliyopita wakati wa Kombe la Dunia. Inasema kuwa timu ya Ujerumani (ya wakati huo) bado haina wachezaji wenye uzoefu wa kutosha, lakini baada ya miaka minne itakuwa timu moja hatari sana. Hili Diego Maradona analitambua kuliko mtu yoyote.
Wednesday, July 7, 2010
Thursday, June 10, 2010
Balozi mpya wa Tanzania Afrika ya Kusini
Balozi mpya anayewakilisha Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Mhe. Radhia Msuya, hivi karibuni aliwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini mjini Pretoria.
Utambulisho huo ulifanyika tarehe 8 Juni 2010 kwenye Makazi ya Rais yaliyopo jijini Pretoria. Rais Jakaya Kikwete alimteua Balozi Musya mwezi Machi mwaka huu kushika nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Emmanuel Mwambulukutu aliyestaafu. Kabla ya uteuzi wake Balozi Msuya aliongoza Idara ya Ulaya na Amerika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Utambulisho huo ulifanyika tarehe 8 Juni 2010 kwenye Makazi ya Rais yaliyopo jijini Pretoria. Rais Jakaya Kikwete alimteua Balozi Musya mwezi Machi mwaka huu kushika nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Emmanuel Mwambulukutu aliyestaafu. Kabla ya uteuzi wake Balozi Msuya aliongoza Idara ya Ulaya na Amerika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Saturday, June 5, 2010
Hii kali
Muda mchache uliopita, Muhidini Michuzi ameripoti kwenye blogu yake kuwa wachawi kumi wanajiandaa 'kuwatengeneza' Brazil kabla ya mpambano na Taifa Stars. Fuatilia hapa:
http://issamichuzi.blogspot.com/2010/06/wachawi-10-wajitokeza-kuiroga-brazil.html
Mimi ushauri wangu huu: bila kushirikisha Muhunda ni kupoteza pesa na muda.
http://issamichuzi.blogspot.com/2010/06/wachawi-10-wajitokeza-kuiroga-brazil.html
Mimi ushauri wangu huu: bila kushirikisha Muhunda ni kupoteza pesa na muda.
Uchaguzi 2010: Eva Sweet Musiba
Mwandishi wa habari wa magazeti ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Sweet Eva Musiba, ni mmoja wa wagombea ubunge wa viti maalum, Mkoa wa Mara, waliyojitokeza kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Maelezo yake ni kama ifuatavyo:
Elimu:
- Stashahada ya Uandishi wa Habari, Dar es Salaam School of Journalism
- Masomo ya Awali ya Uhasibu, Business Efficiency (B.E.I.)
- Darasa la VII, Shule ya Msingi Mwembeni, Musoma
Uzoefu:
- Mwandishi wa habari, Jarida la Mama na Watoto, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mara
- Mhasibu Mwandamizi, kiwanda cha kuchakata minofu ya samaki - Fish Filters Tanzania Limited (Beach Department)
- Mjumbe, bodi ya uandaaji gazeti la TAA la Chama cha Waandishi wa Habari Mwanza (MPC)
- Mteuliwa miongoni mwa waandishi na wapiga picha katika maziko ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Mwitongo, Butiama) 1999
- Mwandishi wa vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na Msanii Afrika (Mwanza), Radio Free Africa (Mwanza), Mzawa (Mwanza), Hoja (Dar es Salaam), TAA (Mwanza), Jarida la Mazingira (Ubalozi wa Sweden), Mwakilishi wa Radio Uhuru Kanda ya Ziwa (2005-2009), Mwakilishi wa gazeti la Uhuru na Mzalendo (2005-2010)
Tuesday, June 1, 2010
Wageni wa Butiama: Walimu toka Canada
Kila mwaka kijiji cha Butiama hupokea wanafunzi wa ualimu toka Chuo Kikuu cha Queen's kilichopo Kingston, Canada. Kwa muda wa majuma kadhaa, wanafunzi hao hushiriki mazoezi yao ya ualimu kwenye Shule ya Sekondari Butiama. Miaka iliyopita walikuwa pia kwenye Shule ya Sekondari ya Machochwe iliyopo Wilaya ya Serengeti.
Pamoja na mazoezi ya kufundisha, wanaleta pia misaada ya vitabu na vifaa vya kufundishia kwenye shule wanazofikia. Chini ya ziara hizi, shule ya Machochwe imepata vifaa vya umeme vinavyotumia nguvu za jua, wakati shule ya Butiama imepokea fedha zilizojenga darasa la wanafunzi.
Kundi la Wakanda la mwaka 2008 (picha ya juu) lilijumuisha wanafunzi waliyotumia muda wao mwingi wa mapumziko wakicheza mpira wa mguu dhidi ya wanafunzi na vijana wa Butiama. Kwenye picha, kutoka kushoto ni Kathleen Bolger, Vicki Bowman, Stacey Copeland, Jennifer Lytle, Jennifer Michel, Shannon Mullins, and Karen Versluys.
Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Canada inashika nafasi ya kumi kwa ubora duniani.
Subscribe to:
Posts (Atom)


