Leo asubuhi, wageni wanne toka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walimtembelea Mama Maria Nyerere kijijini Butiama.
Kutoka kushoto: Col. S.M. Msindo, mwenyeji wao na Mkuu wa Kambi ya JKT Rwamkoma, Lt.Col. Mlawa, Maj. M.M. Kipakulo, Maj. M.P. Kivuyo, na WO2 Daria Malombe. |
Lt.Col. Mlawa, Mkuu wa Kambi ya JKT Rwamkoma akiwapa wageni maelezo nje ya kaburi la Mwalimu Julius K. Nyerere, Mwitongo, Butiama. |
Baada ya kuzuru kaburi la Mwalimu Nyerere, wageni walitembelea Makumbusho ya Mwalimu J.K. Nyerere na kabla ya kuondoka walionana na Mama Maria Nyerere, mjane wa Mwalimu Nyerere.
Wageni pamoja na mwenyeji wao wakiwa pamoja na Mama Maria Nyerere, wa pili kutoka kushoto. |
Wageni hao toka Dar es Salaam walikuwa kwenye ziara ya kikazi.









