Wale ambao wamepata fursa ya kusoma makala zangu za Kiingereza kwenye gazeti la Sunday News watagundua kuwa, mara kwa mara, naandika kuhusu nyoka. Nakutana na nyoka mara kwa mara kiasi ambapo inakuwa vigumu kukwepa hii mada. Wapo kila mahali. Natazama nje ya dirisha langu na naona nyoka anatambaa ukutani (picha ya hapa chini). Kuna mmoja aliingia chumbani kwangu usiku, na nikamkuta sehemu ambapo ninakanyaga niamkapo kitandani.
Kuna safari moja, wakati natoka chumbani kwangu, ikiwa kuna giza kidogo, nilimruka nyoka bila kutambua na nikafunga mlango wa chumba na kumbana nyoka mlangoni. Nilivyorudi chumbani nikamkuta yuko hai, sehemu ya kiwiliwili chake kikiwa nje ya chumba na sehemu ikiwa chumbani kwangu, ingawa alikuwa bado hai. Nilimchota na mti mrefu nikamtoa nje ya nyumba na kumuachia. Kuna mtu aliniuliza: "Kwa nini hukumuua?" Jibu nililipata kwenye asili ya kabila langu: Wazanaki.
Kwanza, angeweza kuwa Muhunda, nilimuarifu, mzimu wa Kizanaki (sisi tunaita musambwa) unaolinda kabila la Wazanaki wa Butiama (kila eneo kati ya maeneo nane ya Uzanaki lina musambwa wake). Tunaamini kuwa Muhunda anaweza kujibadilisha na kuwa nyoka, au chui, au nyani dume. Kwa imani za Wazanaki Muhunda siyo Muumba; Wazanaki wana imani kuwa yupo Muumba na mbingu.
Mimi najiita Mzanaki, japokuwa sina uwezo wa kuongea Kizanaki. Aidha, kwa mujibu wa mila zetu, mimi ni mmoja wa walinzi au wasimamizi wa msitu wa mitambiko ambao nao unaitwa Muhunda, sehemu ambayo Muhunda anaaminika kutembelea mara kwa mara. Kwa hali siyo siwezi kuua kiumbe ambacho napaswa kukilinda, hasa ukizingatia kuwa jukumu kubwa la Muhunda ni kulinda jamii nzima ya wakazi wa Butiama, Watyama.
Mimi naungana na wale wanaoamini kuwa kuna viumbe wachache sana ambao wananaweza kushambulia viumbe wengine bila kuwa na hisia kuwa usalama wao uko hatarini. Ni binadamu pekee ndiyo mwenye hulka ya kushambulia binadamu mwenzake, hata pale ambapo usalama wake hauko hatarini. Nyoka wengi hawashambulii binadamu isipokuwa tu pale wanapohisi kuwa usalama wao unatishiwa, kwa hiyo naamini kuwa sina sababu ya kuua kila nyoka ninayemuona.
Ni nyoka aina ya Mamba Mweusi tu ambaye inasemekana anaweza kumshambulia binadamu pasipo sababu ya msingi.
Thursday, March 1, 2012
Wednesday, February 29, 2012
Wizi wa mitihani ni janga la Taifa
Picha hii (hapa chini) ni ya tangazo lililobandikwa kwenye chuo kimojawapo mashuhuri cha Tanzania kwenye moja ya majiji ya Tanzania.
Nimefuta majina ya walioorodheshwa ili kuhifadhi majina ya wahusika.
Tangazo linaashiria kuwa walioorodheshwa wanatuhumiwa kuibia kwenye mitihani. Mwalimu mmoja ambaye alizisikia taarifa hizi alisema kuwa anaamini kuwa hawa walionaswa ni asilimia ndogo sana ikilinganishwa na wale ambao waliibia lakini hawakunaswa, ambao baada ya muda watahitimu masomo yao.
Kwa nini wizi wa mitihani ni janga la Taifa? Mwalimu Nyerere, katika moja ya hotuba zake, alisema:
Kuna mtaalamu mmoja anasema kuwa tayari tunaongozwa na watu hao.
posted from Bloggeroid

"...[shabaha ya elimu ni] kurithisha kutoka kizazi kimoja had kizazi kingine maarifa na mila za taifa, na kuwaandaa vijana wawe tayari kuchukua nafasi zao katika kulitumikia na kuliendeleza taifa."Kwa mtindo huu, tunarithisha majukumu ya kulitumikia na kuliendeleza taifa kwa wahitimu ambao hawana elimu inayolingana na shahada wanazotoka nazo vyuoni. Ni sawa sawa na kujenga nyumba kwenye msingi hafifu. Kuna siku moja nyumba itaporomoka na tutajikuta tunaongozwa na watu wa mataifa mengine ambapo ipo elimu ya kweli, na wako wasomi wa kweli.
Kuna mtaalamu mmoja anasema kuwa tayari tunaongozwa na watu hao.
Tuesday, February 21, 2012
Salim Mkalekwa kupambana na Abdallah Mohamed (Prince Naseem)
Bingwa wa ndondi za kelipwa wa walterweight (kilo 67) wa Pugilistic Syndicate of Tanzania (PST), Abdallah "Prince Naseem" Mohamed, anatarajia kupanda ulingoni tarehe 24 Februari 2012, katika pambano la ubingwa dhidi ya bondia Salehe Mkalekwa.
Mapambano ya utangulizi yatawahusisha mabondia Shaaban Zungu dhidi ya Hassan Debe (kilo 55); Safari Mbeyu dhidi ya Ibrahim Maokolo (kilo 67); Geoffrey Pacho dhidi ya Dickson Kawiani, na Kulwa Kindondi dhidi ya Khaji Hamisi. Uzito wa mabondia katika mapambano haya mawili ya mwisho haukupatikana.
Pambano hilo linaratibiwa na Shabani "Mwayamwaya" Adiosi na litafanyika kwenye ukumbi wa New Kibeta, Mbagala Kuu, Dar es Salaam.
Picha na taarifa kwa hisani ya Super D Boxing Coach.
| Bondia Salehe Mkalekwa (kushoto), mratibu wa pambano Shabani "Mwayamwaya" Adiosi (katikati), na bondia Abdallah "Prince Naseem" Mohamed (kulia). |
Pambano hilo linaratibiwa na Shabani "Mwayamwaya" Adiosi na litafanyika kwenye ukumbi wa New Kibeta, Mbagala Kuu, Dar es Salaam.
Picha na taarifa kwa hisani ya Super D Boxing Coach.
Thursday, February 16, 2012
Wengine wanakufa kwa njaa, wengine hawataki kula
Zaidi ya mwaka mmoja uliyopita niliona takwimu kwenye wavuti moja inayatoa takwimu za dakika kwa dakika kwa mwaka mzima. Takwimu zilainisha kuwa kwa wakati ule watu 22,000 tayari walikuwa wamekufa kwa njaa duniani na wakati huo huo kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni 22.6 zilikuwa zimeshatumika duniani kote na watu wanaotafuta huduma na dawa za kupunguza uzito.
Hizo pesa zingegawanywa kwa idadi ya watu waliyokufa, kila mmoja angepata zaidi ya Dola milioni moja na kuepusha mtu yoyote kufa kwa njaa.
Tatizo la uzito wa kupindukia ni kubwa kwenye nchi tajiri, lakini haliwezi kuzidi tatizo la kufa kwa njaa linalokabili wakazi wa nchi maskini duniani.

Friday, February 3, 2012
Francis Cheka amshinda Karama Nyilawila kwa pointi
Katika pambano lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro tarehe 28 Januari 2012 bondia Francis Cheka alimshinda Karama Nyilawila kwa pointi katika pambano la uzito wa "Super Middleweight" lisilokuwa la ubingwa.
Katika pambano hilo kali mabondia wote wawili walitupiana makonde ya kujibizana lakini kwa mujibu wa majaji wa mchezo huo, Cheka aliibuka mshindi. Majaji walitoa pointi zifuatazo: John Chagu 100 - 96, Mark Hatia 96 - 97, na Boniface Wambura 99 - 97. Refa wa mchezo alikuwa Nemes Kavishe.
Pambano hilo lilisimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), na promota wa pambano alikuwa Philemon Kyando.
Katika pambano hilo kali mabondia wote wawili walitupiana makonde ya kujibizana lakini kwa mujibu wa majaji wa mchezo huo, Cheka aliibuka mshindi. Majaji walitoa pointi zifuatazo: John Chagu 100 - 96, Mark Hatia 96 - 97, na Boniface Wambura 99 - 97. Refa wa mchezo alikuwa Nemes Kavishe.
| Karama Nyilawila (kushoto) akiinama kukwepa kombora la Francis Cheka katika pambano la hivi karibuni liliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. (Picha kwa hisani ya superboxingcoach) |
Subscribe to:
Posts (Atom)
.jpg)