Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Thursday, August 26, 2010

Michuzi kupanda Mlima Kilimanjaro

Mwamablogu mashuhuri. Muhiddin Issa Michuzi, ameniarifu kuwa ataungana nami mwezi Novemba 2010 kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha pesa za hisani

Michuzi, akiwa na Simba
Tangu mwaka 2008 nimekuwa napanda Mlima Kilimanjaro kwenye tukio linalojulikana kama The Mwalimu Nyerere Charity Climb kwa madhumuni ya kuchangisha pesa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya hisani. Mwaka 2008 nilichangisha zaidi ya dola za Marekani 20,000 kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Chief Edward Wanzagi iliyopo Buturu, Mkoa wa Mara.

Mwaka 2009 nilichangisha pesa kwa ajili ya asasi ya Mjini Musoma, Community Alive, inayosaidia watoto yatima ambao wazazi wao wamekufa kwa UKIMWI. Ahadi na michango vilifikia kiwango kidogo, kulinganisha na mwaka 2009. Ingawa ahadi zilifikia zaidi ya Sh.2 milioni ni sehemu ndogo sana ya ahadi hizo zilitolewa.

Pesa zinazotolewa zinatumwa moja kwa moja kwa walengwa kwenye akaunti zao, na hamna sehemu yoyote inayopunguzwa.

2 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

safi sana! kumbe litakuwa kundi kubwa!!!

Madaraka said...

Hapatatosha kileleni (kama wote waliosema wanakuja watajitokeza). Mimi nilishawahi kumuahidi Jenerali Sarakikya kuwa nitapanda naye Kilimanjaro, lakini ikapita miaka miwili kabla sijapanda.