Enzi za tawala za kitemi, hiyo ndiyo ilikuwa desturi. Mgeni, hasa yule ambaye alikuwa na hadhi ya utawala kama mwenyeji wake, alipigiwa ngoma za mwenyeji wake. Ni ngoma ambazo zilisikika kwenye himaya ya mtemi mwenyeji na zilisambaza taarifa ya kuwepo kwa mgeni muhimu.
Baada ya uhuru wa Tanganyika, desturi hiyo ilihamia kwenye Ikulu ya Dar es Salaam na viongozi mbalimbali waliotembelea Ikulu walipokelewa kwa desturi hiyo.
Rais Nyerere akimkaribisha Rais Sekou Toure wa Guinea kupiga ngoma za kumkaribisha Ikulu, Dar es Salaam. |
Kumbukumbu yangu inaweza kuwa siyo sahihi, lakini sikumbuki kama baada ya Mwalimu Nyerere desturi hii ilifuatwa sana, ingawa tunaona sasa kuwa Rais wa awamu hii ya tano, John Magufuli, ameichangamkia vyema na huwashirikisha viongozi wanaofika Ikulu kupiga ngoma zilizopo Ikulu.
Inawezekana pia kuwa siyo wageni wote wanaofika Ikulu ambao hukaribishwa kwa kupiga ngoma,
No comments:
Post a Comment