Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Thursday, May 20, 2010

Lugha yetu Kiswahili


Picha hii inaonyesha pikipiki ambayo haijapata namba ya usajili yenye maandishi ya lugha isiyokuwepo duniani. Neno "chassis" ni la asili ya lugha ya Kifaransa. Lakini mwenye pikipiki hii, au mwandika namba, ameandika "chasess" neno ambalo haliko kwenye Kiingereza, Kifaransa, wala Kiswahili.

Neno sahihi la Kiswahili lingekuwa "chesisi" kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili - Kiingereza, toleo la pili la mwaka 2000, iliyochapishwa na Taasisi ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa vile msamiati wa Kiswahili unakuwa kila mara, inawezekana limejitokeza neno jingine mbadala linalofanana na lugha yetu. "Chesisi" bado ni neno linalofanana kimatamshi na asili ya lile la Kifaransa.

Ukweli unabaki kuwa katika maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia, kuendeleza ushabiki wa matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye maandishi na mazungumzo ni jambo linalokuwa gumu kila siku zinavyozidi kupita.

Lakini pamoja na hayo bado ni muhimu kuunga mkono jitihada za Serikali kuamua kutumia lugha ya Kiswahili kwenye shughuli zote rasmi za Serikali. Matumaini ni kuwa huu utaratibu utatumika pia bungeni ambapo tabia ya kuchanganya Kiingereza na Kiswahili imekuwa jambo la kawaida.

1 comment:

BLACKMANNEN said...

Kusema kweli "Lugha yetu Kiswahili" inastawi na kuzaa maneno mapya kila kunapokucha. Kama alivyokufafanulia Mzee John Kitime kuwa neno "libeneke" linatokana na aina ya ngoma ichezwayo Morogoro na wewe ukaongezea neno la "rirandi".

Lakini neno lolote jipya la lugha linahitaji kukubalika na wengi kama lilivyo neno la "libeneke". Neno "rirandi" litabidi kusubiri muda mrefu kueleweka kwa wengi na kulikubali kulitumia.

Neno la "ng'wanawane" au wengine wanavyosema kwa makosa "mwanawane" linaenea na kutumika sana na watu. "Ng'wanawane" ni mahusiano ya upendo wa karibu baina ya mzazi na mtoto.

Kwa maana hiyo hiyo, Watanzania wengi wanaolitumia neno hili, wanalisema wakimaanisha mahusiano yao mazuri kati yao na mtu mwingine.

Usahihi wa neno kama lilivyo katika kamusi sio kitu muhimu. Umuhimu unakuwepo katika matamshi. Kwa mfano "Dola" au "Dala". Neno hili limekuja kutoka kwenye filamu za Western Film za Wamarekani.

Matamshi ya Mmarekani kusema "dola" hutamka "dala". Mabasi ya UDA yalipoanza kushindwa kusafirisha watu Dar es salaam, magari ya watu binafsi yalianza (kuchukua abiria vituoni mwa mabasi) kusanya kwa nauli ya senti hamsini hamsini ambayo wao waliita "DALA".

Wasanyaji hawa nauli zao zilikuwa ni flati uwe unateremka karibu au unaenda mbali ilikuwa ni "dala" moja. Hapo ndipo kulikozaliwa neno "daladala".

Kifilamu mtu alipigwa risasi kifuani, lakini bahati alikuwa na fedha ya silva mfukoni mwa shati lake. Risasi ikaipiga senti hiyo na mtu huyo hakufa.

Kipande hicho cha fedha alikishukuru yule mtu, na kukibusu na kusema "One silver dollar saved my Life"=Kipande cha dala moja kimeniepushia kifo. Senti hamsini iliwaepushia adha ya usafiri wasafiri wengi.

It's Great To Be Black=Blackmannen