Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Sunday, May 16, 2010

Teknolojia ya ujenzi wa nyumba ya Hydraform

Kwa miaka kadhaa sasa nchini Tanzania, baadhi ya wajenzi wa nyumba wamekuwa wakitumia mashine za Hydraform kufyatulia matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.


Ujenzi kwa kutumia matofali ya Hydrafom unapunguza matumizi ya saruji inayotumika kwenye ujenzi wa kuta za nyumba kwa sababu matofali hayo yanashikana yenyewe na kuondoa haja ya kuwepo saruji kati ya tofali na tofali. Saruji inatumika kwenye kozi ya kwanza tu ya ujenzi wa ukuta, na kozi tatu za mwisho za ukuta. Kwa sababu hii, matumizi ya saruji ni madogo kuliko kwenye ujenzi wa kutumia matofali ya kawaida.

Aidha. baada ya kumaliza ujenzi wa ukuta, hakuna ulazima wa kupiga ripu kwenye ukuta wa nje. Ripu inapigwa ndani tu na hivyo kupunguza matumizi ya gharama ya saruji kwa ajili ya ripu.


Mashine ya Hydraform inafyatua kati ya matofali 1,300 - 1,500 kwa siku kutegemea na uzoefu wa wafyatuaji. Hata hivyo inawezekana kufyatua hadi matofali 2,ooo kwa siku kwa wafyatuaji wazoefu. Mfuko mmoja wa saruji wa kilo hamsini unatoa matofali kati ya 77 -90, na mchangayniko wa udongo na saruji unatumia maji kidogo sana.

Mchanganyiko hutumbukizwa ndani ya mashine na kushindiliwa kwa nguvu za haidroliki. Matofali yanapotoka kwenye mashine yanapangwa matano matano na kufunikwa kwa siku tatu yakimwagiliwa maji asubuhi na jioni kwa siku hizo tatu. Kuanzia siku ya nne matofali yanaweza kutumika kwa ujenzi.Kutokana na ujenzi wa Hydraform kutotumia saruji kati ya matofali, ujenzi wake ni wa haraka kuliko kawaida.

9 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Wow!!
Hii yaonekana kuwa suluhisho jema saana japo sina hakika kama wazawa wataunga mkono. Ni kwa kuwa twakimbia vya kwetu kutukuza vya wenzetu
Asante kwa uelimishaji huu

deorugz said...

je Hizi mashine Tanzania zinapatikana wapi??

Madaraka said...

Sifahamu zinapatikana wapi Tanzania, lakini wasiliana naao hapa:

http://www.hydraform.com/

Anonymous said...

Mashine zinapatikana NYUMBU KIBAHA.
Sasa mie ningependa kujua bei ya haya matofaliu

Madaraka said...

Bei ya tofali inategemea idadi; idadi ndogo, bei kubwa. Idadi inavyozidi kuongezeka, bei inazidi kupungua.

Adili Liana said...

Ungetuambia inaanzia shilingi ngapi kwa bei ya kawaida na hupungua kwa kiasi gani kama tofali ni nyingi

Madaraka said...

Adili Liana, bei inategemea na eneo na umbali wa sehemu ya kufyatua matofali kutoka umbali wa kupata vifaa kama saruji, udongo, na maji. Ni nadra kwa maeneo kufanana bei.

Amani Urassa said...

Mashine ya hayo matofali ni bei ganii
Na pili kipimo cha maji kidogo ni sawasawa na nn??....

Madaraka said...

Wasiliana na watengenezaji mashine hapa: http://www.hydraform.com/. Maji unachanganya kidogo sana, kwa kunyunyuzia kidogo tu kwenye mchanganyiko wa udongo na saruji.