Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Wednesday, August 4, 2010

Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA ametembelea Butiama leo

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafirishaji, SUMATRA, Israel Sekirasa, leo ametembelea Butiama, akiongozana na Tumaini Silaa, Meneja wa Huduma za Sheria wa SUMATRA.

Israel Sekirasa, kushoto, akiweka sahihi kitabu cha wageni kwenye Maktaba ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Akiwa Butiama alitembelea vivution mbalimbali vya Butiama, ikiwa ni pamoja na maktaba ya Mwalimu Nyerere, Makumbusho ya Mwalimu Nyerere, pamoja na kuzuru kaburi la Mwalimu Nyerere.
Tumaini Silaa (kushoto), na Israel Sekirasa, wakiangalia sehemu ya vitabu zaidi ya 8,000 vilivyo ndani ya maktaba ya Rais mstaafu Mwalimu Nyerere, ambayo inajulikana rasmi kama Maktaba ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

3 comments:

Maisara Wastara said...

Swali: hivi kutembelea mahali hapo kuna kiingilio?

Madaraka said...

Wageni wote wanapaswa kupitia Makumbusho ya Mwalimu J.K. Nyerere, iliyopo hapa Butiama na ambayo iko chini ya mamlaka ya Makumbusho ya Taifa. Huko mgeni analipia kiingilio, lakini anatembezwa mpaka eneo la kaburi la Mwalimu Nyerere.

Nikiwepo mimi, nitakutembeza kwenye maktaba yake ya vitabu zaidi ya 8,000.

Anonymous said...

I hope nitatembelea hvi karibuni Mungu akipenda.