Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Friday, July 30, 2010

Dk Wilbrod Slaa ahutubia Musoma leo

Dk. Wilbrod Slaa, mgombea urais aliyejitokeza kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo hii alihutubia Musoma, akiwa katika ziara fupi ya kupata wadhamini wa kutimiza masharti ya kupitishwa na Tume ya Uchaguzi kama mgombea urais wa chama chake.Katika hotuba yake, Dk. Slaa alisema:
Mwalimu [Nyerere] aliwahi kusema: Ikulu si mahali pa kukimbilia....
Na mara nyingi nimesema, uraisi wa Tanzania hata nikipewa bure, siutaki kwa sababu najua uzito ulioko. Kwa sababu natambua uzito wa maneno ya Mwalimu kuwa hakuna bisahara ya kukimbilia Ikulu. Kwa sababu natambua Ikulu ni dhamana ya kuwabeba Watanzania, kuwasaidia Watanzania walala hoi, wanyonge wasiyo na sauti, kuwanyanyua na kuwapeleka kwenye neema...
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kulia, akimtambulisha mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa
Kwenye mkutano huohuo, mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema:

Watanzania wote wamepigika, na umasikini wenu umaskini wetu ndiyo umekuwa mtaji wa Chama cha Mapinduzi. Chama cha Mapinduzi kina wenyewe, na mwenyewe siyo wewe. Ni kikundi kidogo cha walaji ambao wanatumia utawala wa nchi hii kama neema kwa familia zao, na Watanzania wengine wa kawaida wakiendelea kupigika.

Dk. Slaa, kulia, akimtambulisha mgombea ubunge wa CHADEMA kwa jimbo la Musoma Mjini, Vincent Nyerere

Mabere Marando, akihutubia wakazi wa Musoma
Naye Mabare Marando aliyejiunga na CHADEMA hivi karibuni alisema:

Mwalimu [Nyerere] alituachia maadui watatu: ujinga, maradhi, na umaskini. Sasa ameongezeka adui wa nne: Chama cha Mapinduzi.

Naye Wilfred Rwakatare, mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kagera, ambaye alikuwa kwenye mkutano huo alisema:
Kuna mwana-CCM anaweza akanibishia kwamba kichwa kimoja cha Dk. Slaa ni sawa sawa na wabunge mia moja wa CCM?
Huu ni uchokozi, lakini hatujawasikia CCM nao kujibu mapigo. Bila shaka tutawasikia katika siku zijazo.

3 comments:

nyahbingi worrior. said...

Nimeipenda hii,safi sana.Safari ndio hiyo imeeanza.

John Mwaipopo said...

wakati fulani ukumbi wa siasa ni sehemu tosha kwa kuondoa stress

John Mwaipopo said...

wakati fulani ukumbi wa siasa ni sehemu tosha kwa kuondoa stress