Shabiki wa Chama cha Wananchi (CUF) wa jijini Mwanza akielekea kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu uliyohitimishwa tarehe 31 Oktoba. Mkutano huo ulihutubiwa na Prof. Ibrahim Lipumba, mgombea urais wa CUF.
Thursday, November 4, 2010
Monday, November 1, 2010
Vincent Nyerere wa CHADEMA ashinda ubunge Musoma Mjini
Taarifa rasmi iliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi wa Musoma Mjini, saa 11:30 alfajiri hii, imethibitisha ushindi wa Vincent Nyerere wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa mbunge mpya baada ya kumshinda aliyekuwa mbunge, Vedasto Mathayo Manyinyi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Matokeo rasmi ni haya:
![]() |
Vincent Nyerere, mbunge mteule wa jimbo la Musoma Mjini, akihutubia mkutano wa uchaguzi uliyofanyika Musoma wakati wa kampeni za uchaguzi za zilizoisha juzi. |
Jina la Mgombea
|
Chama
|
Kura Alizopata
|
Asilimia ya Kura
Zote Zilizopigwa
|
Vincent K. Nyerere
|
CHADEMA
|
21,225
|
59.71
|
Vedasto M. Manyinyi
|
CCM
|
14,072
|
39.38
|
Mustapha J. Wandwi
|
CUF
|
253
|
0.71
|
Chrisant N.
Nyakitita
|
DP
|
53
|
0.15
|
Tabu S. Machibya
|
NCCR - Mageuzi
|
19
|
0.05
|
Subscribe to:
Posts (Atom)