Mtanzania Ramadhani Shauri atapanda
ulingoni siku ya Idd pili kupambana na bondia Sande Kizito kutoka Uganda
kugombea mkanda wa IBF katika bara la
Africa katika uzito wa unyoja (Featherweight).
Shauri anayefanya mazoezi yake Ubungo,
Dar es Salaam, maeneo ya Mabibo na anafundishwa na kocha Mzazi anayetamba kuwa na mabondia
wenye nidhamu na vipaji vya hali ya juu.
Ramadhani Shauri ni bondia chipukizi
mwenye umri wa miaka 19 na historia yake ya ngumi inafurahisha kila anayeisoma
na kuisikia. Ana haiba nzuri inayovutia na anafananishwa na bondia Sugar Ray Leonard wa Marekani kutokana
na haiba yake na upiganaji wake.
Sugar
Ray Leonard
alitamba katika miaka ya 70 na 80. Shauri ni Mfalme anayekuja na hivi sasa
anatishia maisha ya mabondia wengi katika bara la Afrika.
Ramadhani Shauri ana nidhamu ya hali ya
juu na maisha yake katika ngumi yanafurahisha kwa jinsi anavyoishi kwa nidhamu
na kufanya mazoezi ya kujijenga katika ngumi. Katika maisha yake anajiepusha
sana na matatizo ambayo vijana wengi wametumbukia kama vile uvutaji wa bangi,
ngono zembe na mambo mengine yasiyo na malengo katika maisha.
Huyu ndiye kweli Mfalme anayekuja katika
ngumi za kulipwa na nchi yetu imepata bahati kubwa sana kuwa na kipaji cha
bondia kama huyu.
Mpambano wa Shauri umepewa jina la “The Rumble in the City of Heaven’s Peace”
(Vurumai katika Jiji la Amani).
Friday, July 20, 2012
Mtanzania Ramadhani Shauri kupambana na Mganda Sande Kizito kuwania ubingwa wa mabara wa IBF Afrika
Labels:
michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment