Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Sunday, April 11, 2010

Boti za Mwanza zinatumia barabara


Kwa watu wenye taaluma ya uandishi wa habari kuna msemo kuwa mbwa anapomuuma binadamu hiyo siyo habari, lakini binadamu anapomuuma mbwa hiyo inakuwa habari ambayo watu wanastahili kufahamishwa.

Katika pitapita zangu jijini Mwanza niliwahi kuona boti imebewa juu ya gari na hii nikaona ni habari ambayo siyo ya kawaida. Kwa hali ya kawaida ni vyombo vinavyopita kwenye maji, kama meli na pantoni, ambavyo hubeba magari.

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hapo sasa kazi ipo Duh! Kwa hiyo na magari yataanza kutembea ziwani au?

BLACKMANNEN said...

Samahani kutoka nje ya "mada". Nimeona kuwa unapenda miziki ya zamani na habari mbali mbali za kihistoria.

Naomba utufahamishe Band ya muziki ya Mara Jazz na mtindo wao wa "Sensera", chini ya aliyekuwa kiongozi wake Juma Nguzo iliishia wapi? Natafuta mtu aliye na kanda au sahani ya nyimbo zao. Nitazinunua kwa gharama yoyote.

This Is Black=Blackmannen

Madaraka said...

Mtaalamu wa muziki ni John Kitime. Ukielekeza hayo maswali kwake, utapata majibu. Mtafute kwenye wavuti yake http://www.mwakitime.blogspot.com/anamuziki Tanzania:

Madaraka said...

Nimekosea kidogo, ni:

http://www.mwakitime.blogspot.com/