Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Saturday, July 17, 2010

Makazi ya Mwalimu Nyerere Butiama

Hii ndiyo nyumba ya Mwalimu Nyerere aliyokuwa akifikia alipokuwa akisafiri kwenda Butiama akiwa kama Rais wa Tanzania kati ya miaka ya sitini hadi miaka ya themanini mwanzoni.

Ni nyumba ambayo ina vyumba vinne. Viongozi wenzake wa wakati huo walipomtembelea Butiama walistaajabishwa na udogo wa nyumba yake, na ndiyo wakafikia uamuzi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kumjengea nyumba nyingine kubwa zaidi ambayo ilijengwa miaka ya themanini katika eneo la Mwitongo.

3 comments:

Anonymous said...

ni Watanzania ama binaadam wachache wataokaoweza kuwa na moyo kama aliokuwa nao huyu Mzee. Nimewahi kufika hapo kama mtalii, swali pekee nililoondoka nalo ni kwa nini Mwalimu uliondoka ukiwa bado kijana? We miss you!

Anonymous said...

Viongozi wetu, hasa Mafisadi waliojaa CCM wanapaswa kutembelea hapa na kujifunza

Anonymous said...

mwalimu tunakukumbuka kwa mengi