Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Wednesday, July 7, 2010

Mada yangu ya leo: Ni nani ataibuka bingwa Kombe la Dunia?

Ni dhahiri kuwa matarajio ya mashabiki wengi wa soka Ulimwenguni, hususani juu ya matokeo ya baadhi ya mechi za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Afrika Kusini sasa hivi, hayajatimia.

Niliweka swali kwenye wavuti hii: "Timu ipi itashinda Kombe la Dunia?" Na ingawa majibu ni machache, yanaakisi yaliyokuwa matarajio ya wengi wanaofuatilia Kombe la Dunia.

Kati ya wasomaji watano wa wavuti hii, wawili walitabiri ushindi kwa Argentina, mmoja kwa Brazil, mmoja kwa Uingereza, na mmoja kwa Hispania. Timu zote hizo nne zimeshafungishwa virago kurudi makwao baada ya kufungwa na timu nyingine zinazoshiriki mashindano ya Kombe la Dunia. Timu ambazo washabiki wengi hawakuzifikiria zimebaki kwenye mashindano. Leo hii, wakati Ujerumani ikijiandaa kupambana na Hispania, ni Uholanzi peke yake iliyopata nafasi ya kuingia kwenye fainali ikisubiri mshindi wa pambano la leo.

Hoja yangu ya leo ni kuwa: utabiri wa nani anaweza kushinda mashindano ya Kombe la Dunia ni jambo gumu sana. Maradona na Argentina walikuwa wanatisha, na Brazil walipoisambaratisha Taifa Stars, tusiokuwa na uzoefu wa soka tuliamini kuwa ndugu zake Marcio Maximo wanaelekea kwenye kutwaa taji.

Lakini, kama ambavyo wataalamu wanasema, matokeo ni baada ya dakika tisini (au mia ishirini, pamoja na penalti).

Nikiulizwa sasa hivi, naitabiria Ujerumani ushindi baada ya kuona ilivyoiadabisha Argentina kwa 4-0. Nimeangalia kumbukumbu niliyonukuu miaka minne iliyopita wakati wa Kombe la Dunia. Inasema kuwa timu ya Ujerumani (ya wakati huo) bado haina wachezaji wenye uzoefu wa kutosha, lakini baada ya miaka minne itakuwa timu moja hatari sana. Hili Diego Maradona analitambua kuliko mtu yoyote.

1 comment:

Blackmannen said...

Japokuwa utabiri wa uhakika ni wa yule "Pweza" na hadi dakika hii niandikapo Pweza huyo hajatabiri.

Mimi natabiri Uholanzi itashinda. Hispania itakuwa imeridhika kufika fainali japo watapenda kushinda.

Sina kigezo kikubwa sana juu ya utabiri wangu huu, mbali ya kusema tu kwamba Waholanzi kidogo wako juu, ninapowalinganisha na Hispania.

This Is Black=Blackmannen