Waathirika wa mafuriko wahame: sehemy ya kwanza kati ya nne
Na Amani Millanga
Ndugu zangu Watanzania, naungana nanyi kutoa mkono wa pole kwa
waathirika wote wa mafuriko. Poleni sana kwa kupoteza ndugu, jamaa, na
marafiki waliofariki katika mafuriko haya. Pia poleni sana kwa kupoteza
mali zenu na vitu vyenu vyote kama nyaraka za umiliki wa nyumba zenu,
vtambulisho na hata picha za familia n.k. ambavyo ni sehemu ya historia
ya maisha yenu. Poleni sana na inshaallah Mungu atawasaidia. Anauona
unyonge wenu. Auona umaskini wenu. Anauona udhalili wenu. Na kubwa zaidi
Mungu muumba anauthamini sana utu wenu enyi waja wake mlioathirika na
mafuriko. Naamuomba Mola Karima aziweke roho za marehemu pema peponi,
inshallah. Nazipongeza jitihada zilizofanywa na watu binafsi, mwashirika
binafsi pamoja na serikali za kutoa msaada wa kila hali na mali katika
kuwafariji waathirika. Inshallah Mungu atakulipeni kwa sadaka zenu.
Wahame Mara Ngapi?
Haya si mafuriko ya kwanza kwa jiji la
Dar es Salaam lakini n mafuriko ya kwaanza kufanya uharibifu mkubwa kama
tulivyoshuhudia. Mafuriko yamefika hadi Ikulu, ofisi za UN na UNDP.
Athari za mafuriko haya zimesababisha kuwepo kwa hoja nyingi kuhusiana
na waathirika. Hoja inayotawala sana kwa baadhi ya watu na vyombo vya
habari ni ile inayosema "waathirika wahame". Hoja hii haina mantiki wala
mashiko yoyote. Hivi kweli hatuoni kwamba tayari waathirika
wamekwishahamishwa na mafuriko? Hawako tena majumbani mwao. wanalala
nje. Hivi tunataka wahame mara ngapi ili hali mvua imeishawahamisha? Kwa
kweli hoja hii ya "wahame" tumeitoa katika wakati usiofaa kabisa. Huu
si wakati wa kuwalaumu na kuwatia hofu ya kuwahamisha waathirika. Huu ni
wakato wa maombolezo, huruma na huduma. Waathirika wanawalilia watoto
zao, ndugu zao na jamaa zao waliofariki. wanalilia mali zao na historia
yao. Kusema "wahame" si uungwana na si utu. Tukumbuke kwamba waathirika
hawakuomba mafuriko. Lakini nitaitumia hoja hii ya "wahame" katika
makala haya kutoa mchango wangu wa nini kifanyike katika wakati huu
mgumu kwa taifa ambalo limesherehekea miaka 50 ya uhuru wake hivi
karibuni.
Hoja za msingi kwa wakati huu: ni namna gani waathirika wanapata
chakula na maji safi na salama; ni namna gani waathirika wanapata vyoo
na bafu; ni namna gani waathirika wanalala; na ni namna gani waathirika
wanapata nguo za kujisitiri; na tumejipanga vipi kuwakinga waathririka
na magonjwa ya kuambukiza ya kipindupindu, malaria, kuhara, minyoo, n.k.
Haya ndiyo mambo muhimu ya kufanywa kwanza. Ingawa baadhi yanafanyika
basi tuongeze juhudi zaidi ya kutoa huduma zaidi. Pili, ni suala la wapi
wanahamia waathirika hawa baada ya Mchikichini. Suala hili linaibua
maswali mengi, lakini baadhi yake ni: Je, wahamishiwe wapi? Je,
tumeishayatenga au kuyapima maeneo hayo ya kuwahamishia waathirika? Je,
tutawalipa fidia za nyumba na ardhi yao? Je, fidia hiyo itachukua muda
gani kumfikia muathirika? Je, wwanza kuhamishwa huko kwenye maeneo mapya
lini? Maswali ni mengi yanayohusu huduma za afya, elimu na jamii huko
wanakohamishiwa maana watu takribani 5,000 si wachache.
Itaendelea.
Tuesday, December 27, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment