Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Friday, March 30, 2018

Jinsi ya kutamka kwa usahihi

Kuna wengi tunapata shida kubwa ya kutamka kwa usahihi maneno na majina - hasa yale ya lugha za kigeni. Au kurudia kuiga jinsi wageni wanavyotamka kwa makosa maneno ya Kiswahili, au majina yetu ya asili.

Siku hizi siyo lazima kujifunza lugha ili kuweza kutamka vyema majina na maneno yanayotokana na lugha za kigeni.

Unaweza kutumia Google Search ukaandika neno unalotaka kujifunza kutamka likitanguliwa na neno la Kiingereza define. Katika ukurasa utakaojitokeza taarifa ya kwanza kabisa itaorodhesha tafsiri ya neno kwa lugha ya Kiingereza ikifuatiwa na alama hii hapa chini.

Image result for audio symbol

Ukibofya kwenye alama hiyo utasikia matamshi sahihi ya neno husika.

Matamshi ya majina yanapatikana kwa wingi zaidi kupitia mtandao wa YouTube kwa kutumia search na kutanguliza "how to pronounce" kabla ya neno jina husika. Mfano: how to pronounce Ngorongoro.

Nimesikia mara nyingi watangazaji wa redio na runinga za Tanzania wakishindwa kutamka majina ya Kiafrika ambayo wasio Waafrika wanayatamka vizuri. Mfano mzuri ni [Rais Emerson] Mnangagwa wa Zimbabwe.

No comments: