Alhamisi iliyopita tuliadhimisha kumbukumbu 11 ya kufariki Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hapa kijijini Butiama. Maadhimisho yalianza na misa iliyoongozwa na Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki, Musoma.
|
Mama Maria Nyerere (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi wa Mkoa wa Mwanza wa Chuo Kikuu Huria, Ben Kapaya (aliyembeba mwanaye, James), akiwa na mkewe (wa pili toka kulia). Siku hiyo ya maadhimisho James alitimiza umri wa mwaka mmoja. |
Baada ya misa ilifanyika sala fupi kwenye kaburi la Mwalimu Nyerere katika eneo la Mwitongo, Butiama.
|
Makongoro Nyerere (kushoto), mwenyekiti wa mkoa wa Mara wa Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwa na Askofu Michael Msonganzila wa Dayosisi ya Kanisa Katoliki ya Musoma (kushoto), pamoja na mgeni toka Uganda, Ssalongo Katumba (katikati). |
Na baada ya sala ya kwenye kaburi wageni walipata chakula cha mchana kwenye makazi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Mwitongo.
|
Makongoro Nyerere (katikati), akiwa na Kisheri Kyanzi Mchere, kiongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UV-CCM), tawi la IFM |
Baadhi ya wageni waliyofika kwenye maadhimisho hayo ni pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Godfrey Ngatuni na mkewe.
|
Mgombea ubunge wa jimbo la Musoma Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Vincent Nyerere (kulia), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Godfrey Ngatuni wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere yaliyofanyika Butiama, tarehe 14 Oktoba 2010. |
No comments:
Post a Comment