Maoni ya Amani Millanga kuhusu mafuriko ya Dar: sehemu ya pili kati ya nne
Kuhamisha bila viwanja na fidia ni dhuluma
Serikali
imetoa mwezi mmoja kwa waathirika kuwa wamehama. Jambo hili si sawa kwa
sababu: kwanza, nyumba ya kuishi haijengwi ndani ya mwezi mmoja kutokana
na waathirika kutokuwa na pesa za kununulia vifaa vya ujenzi katika
hali ya mfuko wa bei na ughali wa maisha ulioko nchini. Pili, tukumbuke
kwamba waathirika tunaowaongelea hapa ni kina mama lishe, wafagia
barabara, walinzi korokoroni, wachimba mitaro, machinga na watu wenye
hali duni. Kipato chao ni kidogo mno hata hawawezi kupata milo mitatu
kwa siku. Ni watu wasio na akiba benki. Ni watu ambao hawawezi kupata
mikopo benki kwani benki haimkopeshi maskini hata siku moja. Na hata
kama wanayo akiba benki lakini ni ndogo sana, haiwezi kujenga nyumba
ndani ya mwezi mmoja ukizingatia ughali wa vifaa vya ujenzi.
Iweje
leo tuwaambie waondoke wakajenge nyumba ili hali tunajua fika kwamba
hawana uwezo wa kujenga nyumba? Tatu, ipo hoja kwamba waathirika
waliwahi kupewa viwanja wakati Mzee Makamba akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam nao wakaviuza. Hawakuhama. Na sasa tunawalaumu kwa kuacha kuhama
wakati ule. Lakini tusisahau kwamba waathirika hawa wameishi katika
maeneo haya kwa miaka mingi sana. Hawakuhamia jana wala juzi. Wana
historia ya vizazi na vizazi. Mtu kazaliwa pale, kakulia pale, kaoa au
kuolewa pale na sasa ana wajukuu tunamwambia ahame eti aepuke mafuriko
(ambayo hayatokei kila mwaka) bila kulipwa fidia. Hivi hoja hii
itakuingia akilini hata kama ni wewe? Kama ni mimi sihami ng'o.
Waathirika walipaswa kulipwa fidia ya nyumba zao ili kupitia hapo
wapate nguvu ya kifedha ya kuwawezesha kwenda kujenga huko waendako.
Naamini hakuna mwathirika hata mmoja aliyewahi kulipwa fidia enzi za
Makamba akiwa mkuu wa mkoa ili ahame. Sasa kama hawakulipwa fidia kwa
nini leo tunawalaumu? Uko wapi utu katika suala hili? Iko wapi sheria
inayolinda haki na utu wa waathirika hawa?
Nafahamu
kabisa kuwa serikali au jiji litatumia mabavu kuwahamisha waathirika
kwani limewahi kufanya hivi mara nyingi tu na kuwahamisha watu. Niseme
wazi kabisa, kwamba, kitendo cha kuzibomoa nyumba za waathirika bila
fidia inayolingana na thamani ya eneo hilo lililoko katika jiji, na bila
kuwapa viwanja, kitakuwa ni kitendo cha dhuluma. Na pia kuwapa viwanja
tu, au kuwalipa fidia tu, ni dhuluma vilevile. Tutakuwa tumefanya
uonevu. Tutakuwa tumekiuka haki za binadamu. Tutakuwa tumeudhalilisha
utu wa waathirika. Baya zaidi tutakuwa tumewafanya waathirika kuwa
maskini zaidi na zaidi.
Tukumbuke kuwa wakati wanajenga
serikali ilikuwepo. Mbona haikuwazuia? Bomoabomoa ikifanyika bila
kuwatendea haki itakuwa ni udhalimu. Katika hali sasa upo uwezekano wa
kutolewa hoja kwamba serikali haiwezi kuwalipa fidia waathirika
wanaoishi mabondeni. Swali hapa ni kama ni halali kuilipa Dowans zaidi
ya shilingi bilioni 94, iweje haramu kuwalipa waathirika?
Kimsingi
huenda pesa watakayolipwa waathirika isifikie hata robo ya malipo ya
Dowans. Kivipi? Wako waathirika takriban 5,000. Ukiwa na wastani wa watu
watano kwa familia moja ina maana una familia 1,000 za waathirika
ambazo ni kaya au nyumba 1,000. Tuseme tunawalipa shilingi milioni 20
kila familia. Unapata jibu kwamba ni shilingi milioni 20 zidisha kwa
familia 1,000 ambazo ni jumla ya shilingi bilioni 20.
Pesa
hizi zitabaki nchini hazitakwenda nje kama Dowans. Pesa hizi zitaondoa
umaskini kwa waathirika kinyume na zile za Dowans zitakazoongeza
umaskini kwa kila mtanzania. Shilingi bilioni 94 ukizigawa kwa watu
milioni 43 tulionao sasa utapata kila mmoja wetu analipa shilingi
2,186.05. Asilimia 50 ya Watanzania kwa mujibu wa takwimu zetu ni
maskini wanaoishi chini ya dola moja kwa siku. Dola moja ni sawa na
shilingi 1,583.50 leo hii tunawataka kila mmoja alipe dola 1.38 sawa na
shilingi 2,186.05 kwa Dowans. Kama mlo wa Mtanzania maskini ni shilingi
1,000 kwa siku basi hii ina maana kwamba maskini wasile siku mbili ili
tukawalipe Dowans. Ajabu sana hii.
Itaendelea.
Saturday, December 31, 2011
Tuesday, December 27, 2011
Maoni ya Amani Millanga kuhusu mafuriko ya Dar: sehemu kwa kwanza kati ya nne
Waathirika wa mafuriko wahame: sehemy ya kwanza kati ya nne
Na Amani Millanga
Ndugu zangu Watanzania, naungana nanyi kutoa mkono wa pole kwa waathirika wote wa mafuriko. Poleni sana kwa kupoteza ndugu, jamaa, na marafiki waliofariki katika mafuriko haya. Pia poleni sana kwa kupoteza mali zenu na vitu vyenu vyote kama nyaraka za umiliki wa nyumba zenu, vtambulisho na hata picha za familia n.k. ambavyo ni sehemu ya historia ya maisha yenu. Poleni sana na inshaallah Mungu atawasaidia. Anauona unyonge wenu. Auona umaskini wenu. Anauona udhalili wenu. Na kubwa zaidi Mungu muumba anauthamini sana utu wenu enyi waja wake mlioathirika na mafuriko. Naamuomba Mola Karima aziweke roho za marehemu pema peponi, inshallah. Nazipongeza jitihada zilizofanywa na watu binafsi, mwashirika binafsi pamoja na serikali za kutoa msaada wa kila hali na mali katika kuwafariji waathirika. Inshallah Mungu atakulipeni kwa sadaka zenu.
Wahame Mara Ngapi?
Haya si mafuriko ya kwanza kwa jiji la Dar es Salaam lakini n mafuriko ya kwaanza kufanya uharibifu mkubwa kama tulivyoshuhudia. Mafuriko yamefika hadi Ikulu, ofisi za UN na UNDP. Athari za mafuriko haya zimesababisha kuwepo kwa hoja nyingi kuhusiana na waathirika. Hoja inayotawala sana kwa baadhi ya watu na vyombo vya habari ni ile inayosema "waathirika wahame". Hoja hii haina mantiki wala mashiko yoyote. Hivi kweli hatuoni kwamba tayari waathirika wamekwishahamishwa na mafuriko? Hawako tena majumbani mwao. wanalala nje. Hivi tunataka wahame mara ngapi ili hali mvua imeishawahamisha? Kwa kweli hoja hii ya "wahame" tumeitoa katika wakati usiofaa kabisa. Huu si wakati wa kuwalaumu na kuwatia hofu ya kuwahamisha waathirika. Huu ni wakato wa maombolezo, huruma na huduma. Waathirika wanawalilia watoto zao, ndugu zao na jamaa zao waliofariki. wanalilia mali zao na historia yao. Kusema "wahame" si uungwana na si utu. Tukumbuke kwamba waathirika hawakuomba mafuriko. Lakini nitaitumia hoja hii ya "wahame" katika makala haya kutoa mchango wangu wa nini kifanyike katika wakati huu mgumu kwa taifa ambalo limesherehekea miaka 50 ya uhuru wake hivi karibuni.
Hoja za msingi kwa wakati huu: ni namna gani waathirika wanapata chakula na maji safi na salama; ni namna gani waathirika wanapata vyoo na bafu; ni namna gani waathirika wanalala; na ni namna gani waathirika wanapata nguo za kujisitiri; na tumejipanga vipi kuwakinga waathririka na magonjwa ya kuambukiza ya kipindupindu, malaria, kuhara, minyoo, n.k. Haya ndiyo mambo muhimu ya kufanywa kwanza. Ingawa baadhi yanafanyika basi tuongeze juhudi zaidi ya kutoa huduma zaidi. Pili, ni suala la wapi wanahamia waathirika hawa baada ya Mchikichini. Suala hili linaibua maswali mengi, lakini baadhi yake ni: Je, wahamishiwe wapi? Je, tumeishayatenga au kuyapima maeneo hayo ya kuwahamishia waathirika? Je, tutawalipa fidia za nyumba na ardhi yao? Je, fidia hiyo itachukua muda gani kumfikia muathirika? Je, wwanza kuhamishwa huko kwenye maeneo mapya lini? Maswali ni mengi yanayohusu huduma za afya, elimu na jamii huko wanakohamishiwa maana watu takribani 5,000 si wachache.

Monday, December 26, 2011
Matumla na Maneno nguvu sawa
Mabondia Rashidi 'Snake Man' Matumla, na Oswald 'Mtambo wa Gongo' Maneno wametoka sare katika pambano lao la jana lisilo la ibingwa kwa kugawana pointi 99 kwa 99.
![]() |
Rashidi Matumla, kushoto, anakwepa ngumi ya Maneno Oswald katika pambano la jana. |
![]() |
Rashidi Matumla akiamka baada ya kuteleza kwenye pambano la jana. |
Bila shaka tutasikia mpambano mwingine kati ya hawa mabondia wawili.
Picha na baadhi ya taarifa kwa hisani ya www.superdboxingcoach.
Saturday, December 24, 2011
Mabondia Rashidi Matumla na Oswald Maneno wapima uzito tayari kwa pambano lao kesho
Mratibu wa pambano za ngumi za kulipwa Shabani Adios "Mwayamwaya', katikati, akishuhudia mabondia Maneno Oswald "Mtambo wa Gongo", kushoto, na Rashidi 'Snake Man' Matumla kulia, wakitunishiana misuli mara baada ya kupima uzito leo kabla ya pambano lao lisilo la ubingwa litakalofanyika Dar es Salaam siku ya Noeli kwenye ukumbi wa Heineken, Mtoni Kijichi.
Picha na habari kwa hisani ya www.superdboxingcoach. blogspot.com
Picha na habari kwa hisani ya www.superdboxingcoach.
Subscribe to:
Posts (Atom)