Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Wednesday, May 22, 2013

Tatizo la ziara ya Rais Obama Tanzania

Rais Barack Obama akija Tanzania sina hakika kama atafika Dar es Salaam, lakini iwapo atafika huko mimi nitafanya jitihada niwe sehemu nyingine ya Tanzania. Nakumbuka Rais George Bush alipotembelea Dar es salaam na sitaki yanikute ya wakati huo.

Kero kubwa ilikuwa kufungwa kwa barabara kuu za Dar es Salaam kwa muda mrefu kupisha msafara wa Rais Bush na mwenyeji wake kuelekea Ikulu. Yaliyojiri Ikulu sifahamu lakini nakumbuka kuona picha moja ikionyesha wanajeshi wa Marekani wakiwa juu ya paa la Ikulu wakipiga doria kali kumlinda Rais wao kwenye eneo la Ikulu yetu.

Bila hata kutembelewa na rais wa Marekani, jiji la Dar es salaam linafikiwa na waheshimiwa wengi tu wazalendo ambao kila wanapopita kwenye barabara zake basi husimamisha matumizi ya barabara zake kwa wakazi wa Dar es Salaam. Atakapofika Mheshimiwa Obama ni dhahiri kuwa yatatokea yale yale ya aliyemtangulia au hata zaidi.

Ilipotua ndege ya George Bush kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ndege nyingine hazikuruhusiwa kutumia uwanja huo mpaka ilipoondoka. Watanzania ambao kawaida huongoza ndege zinazotumia uwanja wa ndege wa Dar es Salaam walipewa likizo ya muda na kazi yao ilikasimiwa na wageni mpaka ndege ya rais wao ilipopaa. Rais Bush alipokwenda Arusha mawasiliano ya simu za viganjani yalikatwa kabisa mpaka alipoondoka.

Ninegombwa ushauri ningesema Rais Obama asifikie Dar es Salaam ambako ataathiri shughuli za watu zaidi ya milioni 4. Afadhali aende hata Dodoma. Au aje Butiama, ambako kuna wakazi wasiozidi 20,000.

1 comment:

Gerald Nyerere said...

Kweli Mada, ila kwa kuwa anakuja na msafara wa watu 1,200 wakiwemo wafanya biashara 500. Ingekuwa vizuri hao wafanya biashara ndiyo wakawa Dar es salaam na msafara wake ukawa Dodoma, na hata kutembelea Butiama.