Kombe la Dunia la FIFA limeisha hivi karibuni na nilisikia (kwenye redio na runinga) na kuona kwenye maandishi, haswa kwenye mitandao ya jamii, matumizi yasiyo sahihi ya majina ya baadhi ya timu zilizoshiriki kwenye mashindano hayo.
"Ujerumani" iliandikwa "Ujeruman." Na kwa Kiingereza badala ya kuandika "Germany", baadhi ya watu waliandika "German." Tatizo hili la matumizi ya lugha lisichukuliwe kuwa ni kwa lugha au majina ya kigeni pekee. Jana nikiwa kwenye ndege nilisikia mfanyakazi wa ndani ya ndege akitutangazia abiria kuwa "tumetua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerele." Huyo ni Mtanzania anashindwa kutamka "Nyerere." Na haikuwa mara yangu ya kwanza kusikia "Nyerere" kuitwa Nyerele." Kama ungeondoa muktadha ungefikiri alikuwa anazungumzia nyenyere.
Lakini jambo la kushangaza zaidi ni kuwa baada ya kutamka hivyo alianza kuongea kwa Kiingereza kutoa taarifa hiyo hiyo kwa abiria tuliokuwa ndani ya ndege, lakini alipoongea kwa Kiingereza alitamka "Nyerere" kwa usahihi.
Nilipanda ndege ya shiriki hili. Safari ilikuwa nzuri, lakini lugha ilikuwa na walakini. |
Nawasilisha hoja.
2 comments:
mkuu hiyo unazungmzia kwenye kuzungumza, ila kwenye kuandika ni tatizo kubwa sana niliwa kwenda kwenye hotel moja nzuri kabisa Arusha public relations officer wake ambaye ni binti wa kichagga anaflow Kiingereza huwezi amini kwamba ni mbongo lakini ilipokuja kwenye kuandika akaniandikia kwamba this is the WRITE place to bring your visitors, you are most welcome!
Hii kweli mpya!!!
Post a Comment