TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) imetoa
kibali kwa bondia wa kimataifa wa Tanzania Francis Miyeyusho kucheza pambano la
ngumi nchini Uingereza. Miyeyusho atazipiga na bondia Luke Wilton wa Uingereza
tarehe 27 mwezi huu katika hoteli ya Holiday Inn iliyo katika mtaa wa jijini
Belfast, Ireland ya Kaskazini. Mpambano huo ni wa kugombea mkanda wa kimataifa
wa Masters katika uzito wa Super Fly.
Miyeyusho anatarajia kuondoka nchini tarehe 22 mwezi
huu siku ya Jumapili na shirika la ndege la Uingereza (British Airways).
Francis Miyeyusho ni bondia wa kimataifa aliye kwenye
viwango vya mashirikisho / vyama mbalimbali ya vya ngumi duniani. Shirikisho
la ngumi la Kimataifa IBF limemweka kwenye nafasi ya 5 katika orodha ya
mabondia 15 bora wa mabara duniani.
Hii ni mara ya kwanza kwa Francis Miyeyusho kucheza
nchini Uingereza na mabondia wa huko na anatagemea kuonyesha umahiri mkubwa
katika mpambano huo.
TPBC inamtakia
safari njema Miyeyusho katika safari yake ya kuitangaza Tanzania katika medani
ya michezo ya kimataifa.
Ikumbukwe kwamba ni Ngumi za Kulipwa pekee ambazo
zimekuwa zinaig’arisha na kuitangaza vyema Tanzania katika miaka ya karibuni.
Katika mpambano huo, wimbo wa Taifa la Jamhuri ya
Muungano wa Tanznaia utapigwa mbele ya maelfu ya watazamaji pamoja na
mamilioni wengine ambao watakuwa wanaangalia kwenye luninga.
TPBC imeanzisha rasmi mkakati wa kutumia mchezo wa
ngumi za kulipwa kuitangaza Tanzania kama sehemu salama ya kufikia kwa watalii
na wawekezaji (destination market for tourism and direct investments)
"Sports Tourism" kwa maana ya "Utalii wa Michezo"
Aidha tunamuombea Mungu Miyeyusho aende salama na
afanikiwe kurejea na mkanda wa International Masters nchini Tanzania.
Imetolewa na:
Onesmo
A.M.Ngowi
Rais,
Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)
No comments:
Post a Comment