Kwenye kura zilizopigwa tarehe 1 Aprili 2012, CCM kimeshindwa kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru
lililoachwa wazi kutokana na kifo cha mbunge wake, Jeremiah Sumari, ambaye
alikuwa mwanachama wa CCM.
Kwamba wapiga kura walewale waliyomchagua mwanachama wa CCM
kuwa mbunge wao mwaka 2010 wameamua sasa kuchagua mgombea wa CHADEMA ni ishara
dhahiri kuwa CCM inaendelea kupoteza imani ya Watanzania wengi.
Ni mwanzo wa mwisho wa CCM kama chama tawala? Tuanze mazoezi
ya kumwita mwanachama wa chama cha upinzani “Mheshimiwa Rais”? Jibu litategemea
iwapo CCM kitajiangalia upya na kuirejesha misingi ambayo ilikifanya kuwa chama
kilichopigania maslahi ya wakulima na wafanyakazi. Baada ya hilo, itategemea
kwa kiasi kikubwa nani atateuliwa na CCM kuwa mgombea wa urais kwenye uchaguzi
mkuu ujao wa 2015.
CCM wakiendelea na muenendo wao wa sasa, muda si mrefu watahamia
kwenye benchi za upinzani bungeni.
No comments:
Post a Comment