TAARIFA
KWA UMMA
FEBRUARY 6, 2013
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Bingwa wa IBF katika bara la Afrika uzito wa unyoya (Featherweight) Ramadhani Shauri amepewa nafasi ya kugombea ubingwa wa dunia wa IBF kwa vijana walio chini ya miaka 25 katika uzito wa Lightweight. Shauri ambaye alishinda taji la ubingwa wa IBF katika bara la Afrika mwaka jana baada ya kumpiga bondia Sunday Kizito wa Uganda ana rekodi ya mapambano 17.
IBF
imeamua kumpatia Shauri nafasi ya kugombea ubingwa huo wa dunia kwa vijana
baada ya kuangalia mkanda wa video wa pambano lake la ubingwa wa Afrika na
kuridhika kuwa anaweza kushindania ubingwa huo wa vijana,
Mabondia
wengi wa Marekani ambao walikuja kuwa mabingwa wa dunia na kuweza kupata pesa
nyingi walianza kuwa mabingwa wa dunia kwa vijana na hivyo kuweza kupanda chati
kwenye viwango vya IBF. Mbondia hao ni kama Bernard Hopkins, Floyd Mayweather
na Oscar De la Hoya.
Ramadhani shauri akiwa na mkanda wa ubingwa wa IBF Afrika. |
Kama
Shauri atashinda na kuwa bingwa wa dunia upande wa vijana atakuwa kwenye macho
ya mapromota wakubwa duniani kama kina Dong King, Bob Arum na wengine wengi.
Nafasi kama hii inaipa nchi ya Tanzania nafasi nzuri sana ya kujitangaza
kibiashara na utalii kwani dunia inaiona kuwa kati ya nchi zinazotoa mabingwa
wa dunia.
Kama
Shauri atashinda taji hili atakuwa Mtanzania wa kwanza tangu historia ya ngumi
nchini kuweza kushinda taji la shirikisho kubwa kati ya manne duniani ambayo ni
IBF, WBA, WBO na WBA.
Shirikisho
la Ngumi la Kimatafia Afrika (IBF/Africa) ambalo lina makao yake makuu ya
kuhudumia bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ndilo
lililomtafutia Shauri nafasi aliyopata.
IBF/Africa
inawahamasisha Watanzania walio na mapenzi mema na nchi yao pamoja na makampuni
mbalimbali binafsi ya umma yajitokeze kwa wingi kumpatia Shauri ufadhili wa
kuweza kuligombea taji hili.
Mungu
mbariki bondia Ramadhani Shauri, Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amen.
Imetolewa na:
UTAWALA
Shiriklisho la Ngumi la Kimataifa Afrika (IBF/Africa)Dar-Es-Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment