Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Tuesday, February 5, 2013

Mada yangu ya leo: Tulipie gazeti na kupanga kurasa?

Mara kwa mara hununua gazeti na ninapoanza kusoma nakuta kuwa kurasa za ndani hazijapangwa kwa mtiririko wa kawaida, namba za mwisho zikiwa zimetangulia. Mathalani, unaweza kusoma kurasa ya tano na ukiendelea unakuta inafuata kurasa ya 19.

Hii inatokana na mpangilio mbaya wa karatasi zilizomo ndani zenye kurasa nne kila moja. Ni rahisi kurekebisha huu mkanganyiko kwa kupanga vyema tu hizo kurasa na kuendelea kusoma gazeti kwa mtiririko uliyokusudiwa na wahariri.

Kwa hiyo mara kwa mara hujikuta najaribu kurekebisha huo mpangilio uliokusudiwa na naamini wasomaji wengine wengi hufanya hivyo. Hii ni kazi ambayo inapaswa kufanywa na wachapishaji lakini ni dhahiri kuwa hawaifanyi, au kwa kuona haina umuhimu, au yawezekana kuwa mashine ambazo zinapaswa kufanya kazi hii ya kupanga kurasa hazifanyi kazi vizuri.

Kwa sababu yoyote iliyopo ni suala ambalo halipaswi kuendelea. Mteja alipie gazeti, halafu apange kurasa za gazeti? Hii ni bidhaa ambayo haijakamilika. Haina tofauti na kwenda kwa kinyozi halafu akukabidhi mashine ya kunyolea nywele na kukwambia ukate nywele zako mwenyewe halafu ukimaliza akudai hela.

1 comment:

Anonymous said...

Mkuu,

Baba Mkwe wangu ni mwanahabari. Nilipokuja likizo TZ mwaka 2009 aliniomba nikirudi nimletee magazeti ya kila siku ya TZ. Nikamnunulia magazeti kibao nikamletea.

Baada ya siku kadhaa akanialika tupate sip. Baada ya kupata sip za kutosha akaanza kuzungumzia aliyosoma kwenye magazeti na kuniuliza maswali. Baadaye akaanza kuzungumzia aliyoyasoma, mitindo ya uandishi aliyoiona, uchapishaji wa magazeti, quality za makaratasi na mpangilio wa magazeti yenyewe. Kwa kweli nilijilaumu sana kwa nini nilipotea step na kumletea yale magazeti!