William Rutta ni Meneja wa Kiroyera Tours. Hapa anatoa maelezo kuhusu utamdauni wa kabila la Wahaya wa kula senene.
*************************************************
Senene katika utamaduni wa Wahaya
William Rutta |
na William Rutta
Senene (Ensenene, kwa Kihaya) ni miongoni mwa wadudu wanaotumiwa sana na
kabila la Wahaya mkoani Kagera kama kitoweo, pengine kuliko kabila lolote tangu
enzi za mababu.
Pamoja na wadudu hao kuheshimika katika kabila la Wahaya, historia kamili ya asili ya wadudu hao bado haijulikani.
Mwanzoni senene waliliwa na wanaume peke yake. Wanawake walionywa
wawe na haya siku zote na wasivunje mwiko kwa kula senene na vitu vyote
vilivyokatazwa. Wanawake wote walikuwa na utii wakiheshimu mila na desturi za
kabila lao hivyo kutokana na haya hiyo waliitwa “WAHAYA”.
Wasichana walipeleka
zawadi ya senene kwa wachumba wao kama ishara ya kuonyesha upendo na utayari wa
kuolewa na mchumba huyo. Msichana ambaye hakufanya hivyo uwezekano wa kuolewa na
mchumba wake ulikuwa mdogo, hivyo senene walitumika kama ishara ya upendo na
uaminifu.
Zipo aina nyingi za senene lakini wale wanaozungumziwa hapa
wamegawanyika katika kundi lijulikanalo kama Orthopterous. Hawa ni jamii ya
panzi wapole ambao hawana tabia ya kuharibu na kuteketeza makazi yao kwa
chakula kama walivyo nzige wengine. Senene huzaliana kwa wingi katika mwambao
wa maziwa makuu baada ya kutaga mayai yao ardhini kipindi cha kiangazi.
Baada ya kutaga mayai na kuangua mzunguko wa maisha yao huishia
kati ya mwezi Oktoba na Desemba ambapo kipindi hiki huwa ni msimu wa mvua za
vuli zijulikanazo kwa wahaya kama Omusenene. Hiki ni kipindi ambacho senene
huruka wakiwa katika makundi wakihitimisha safari ya maisha yao.
Pamoja na kutumika kama kitoweo pia jamii imeanza kufaidika na
senene kama chanzo cha kujipatia kipato, jambo ambalo limeufanya mkoa wa Kagera
hasa Bukoba kujulikana sana kitaifa na kimataifa, pia kutokana na uchunguzi wa
madaktari imeonekana kuwa senene wanaongeza vitamin “C”
Taarifa nyingine inayofanana na hii:
http://muhunda.blogspot.com/2011/09/lugha-yetu-kiswahili.html
Taarifa nyingine inayofanana na hii kutoka kwenye blogu yangu ya lugha ya Kiingereza
http://madarakanyerere.blogspot.com/2012/10/akamwani-traditional-welcome-gesture-in.html
3 comments:
makala yako ni nzuri sana,ila sijaelewa uliposema hutaga mayai yao ardhini,naomba unifafanulie ni ardhi ipi hasa na mifano ya maeneo husika
Senene hutaga mayai yao hasa hasa kandoni mwa maziwa makuu hasa upade wa Magharibi mwa Ziwa Victoria hasa kwenye maeneo ya michanga oevu.
Karibu
William Rutta
Safi sana...
Post a Comment