Juzi nimeanza rasmi maandalizi (ya mazoezi) ya kukwea tena Mlima Kilimjaro mwezi Septemba mwaka huu, kuanzia tarehe 23 hadi 30 Septemba. Safari hii nitakuwa nachangisha pesa kuchangia ujenzi wa shule ya msingi iliyopo kijiji cha Kichalikani, mkoa wa Tanga. Yanahitajika mazoezi ya siyo chini ya miezi mitatu kujiandaa vyema kukabiliana na changamoto ya kufika kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, mita 5,895 juu ya usawa wa bahari.
Hii ni safari ambayo awali nilipanga ifanyike mapema mwaka huu lakini nililazimika kuiahirisha kutokana na majukumu mengine yaliyonikabili.
|
Mandhari mwanana kwenye njia ya Marangu ya Mlima Kilimanjaro. |
Moses Kusotera, raia wa Zimbabwe anayeishi na kufanya kazi nchini Uingereza, ataungana nami kukwea mlima huu maarufu pamoja na kuchagnisha pesa za shule ya Kichalikani.
Ukitaka kujiunga nami niandikie barua pepe kwa kubofya
hapa.
Taarifa nyingine zinazohusiana na hii:
http://muhunda.blogspot.com/2013/01/kunguru-wa-mlima-kilimanjaro.html
http://muhunda.blogspot.com/2011/07/wagumu-wa-mlima-kilimanjaro.html
No comments:
Post a Comment