Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Saturday, March 6, 2010

Kumbukumbu ya ajali ya ndege

Kabla ya kuanza vita vya Kagera kati ya Tanzania na Uganda mwaka 1979 na wakati wa maandalizi ya kuanza mapambano hayo ilitokea ajali ya ndege ya Jeshi la Wanancnhi wa Tanzania (JWTZ) iliyosababishwa na kutunguliwa kwa makosa kwa ndege mbili zilizokuwa zikihamishwa kutoka kambi ya Ngerengere kwenda Mwanza.

Kutokana na kasi ya hizo ndege marubani wawili walivyofika Mwanza walijikuta wamepitiliza na katika jitihada za kurudi tena kutua Mwanza, ndege hizo zilipita kwenye anga ya Musoma ambapo zilitunguliwa na mizinga ya JWTZ kwa makosa kwa sababu ya kutokuwa na taarifa juu ya kupita kwa ndege hizo kwenye anga ya Musoma na kudhaniwa kuwa ni ndege za jeshi la anga la Uganda.

Baada ya kushambuliwa, ndege moja ilianguka Musoma na nyingine iliangukia Butiama, pembezoni mwa msitu wa Muhunda, na zaidi ya kilomita 40 toka Musoma. Sehemu ilipoanguka ndege hiyo ndiyo imewekwa kumbukumbu hii.
 
 Hii kumbukumbu ilijengwa miaka kadhaa iliyopita, lakini jambo la ajabu ni kuwa hivyo vyuma vinavyoonekana pembeni vilibanduliwa na wafanyabiashara wa vyuma chakavu kwa ajili ya kuuza kwenye viwanda vinavyotengeneza nondo.

2 comments:

Anonymous said...

HABARI HII NI NZURI SANA. LAKINI IMEPUNGUA UZURI KWA KUKOSEKANA JINA LA RUBANI AYEKUWA AKIIRUSHA.

Madaraka said...

Ni kama vile ulisoma mawazo yangu. Leo hii nimetoka kumwambia afisa mmoja wa Jeshi kuwa nimejaribu kwa muda mrefu kupata jina hilo ili liweze kuwekwa pale kwenye ule mnara.

Mimi mwenyewe, hivi karibuni nilikuwa Dar na kwa mara ya pili niliomba kupata hiyo kumbukumbu lakini mpaka sasa hivi sijafanikiwa.

Lakini naamini kuwa JWTZ wataona umuhimu huo ambao wewe pia umeuona ili wageni wanaotembelea kumbukumbu hii waweze kufahamu hilo jina.