Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Saturday, June 11, 2011

Takwimu: Majeshi ya Libya na Syria*

Ukilinganisha majeshi ya Syria na Libya, unaweza kupata picha ni sababu gani moja kuu ambayo inafanya jumuiya ya Kimataifa kuishamblia Libya bila woga lakini kujiumauma meno kuhusu suala la kuichukulia hatua kama hizo Syria kwa shutuma dhidi ya kile kinachoelezwa majeshi ya nchi hizo mbili kushambulia raia wake.


Libya
Syria
Askai wa Miguu


Askari
76,000
325,000
Mgambo na askari wa akiba
40,000
314,000
Vikosi vingine vya kijeshi (kama FFU)
0
108,000
Jumla
116,000
747,000Zana za Kijeshi


Vifaru
1,540
4,600
Mizinga ya kutungua ndege
600
6,385
Ndege za kivita
447
607
Idadi ya wanajeshi na zana peke yake siyo kipimo sahihi cha nguvu ya jeshi, lakini ni dhahiri kuwa kuishambulia nchi yenye askari 108,000 ni rahisi zaidi kuliko kushambulia nchi yenye askari 747,000.

*Taarifa zinatokana na wavuti hii hapa, na hii.

1 comment:

Madaraka said...

Tofauti na hoja yangu kuwa kikwazo cha kuvamia Syria ni ukubwa wa majeshi yake, kuna mtaalamu wa masuala ya usalama anayeeleza hapa http://www.stratfor.com/weekly/jihadist-opportunities-syria kuwa kinachowaogopesha wakubwa ni uwezekano wa uvamizi wa Syria kijeshi kuchochea mazingira ambayo yatavuruga amani katika eneo kubwa kuvuka mipaka ya Syria yenyewe na hatari ya kuingiza mataifa mengine katika vita.