Muda si mrefu uliyopita nilipokea simu ikiniarifu kuwa kuna mgeni amefika nyumbani. Nilipouliza ni nani, niliambiwa: "Profesa Mbilinyi."
|
Profesa Simon Mbilinyi (kulia) akijaza kitabu cha wageni kwenye maktaba ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo kwenye makazi ya Mwalimu Nyerere, Butiama. Katikati ni Profesa Marjorie Mbilinyi. |
Nikielekea kuonana na mgeni nikawa najiuliza: "Huyu atakuwa Profesa Mbilinyi yupi? Hakuwa mmoja, walikuwa wawili: Profesa Marjorie Mbilinyi, na Profesa Simon Mbilinyi (ambaye ni mume wake) ambao walikuwa wamepita Butiama wakielekea Ukiliguru ambapo waliwahi kufanya kazi zamani.
Profesa Marjorie Mbilinyi ni mwanaharakati wa masuala ya jinsia na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Profesa Simon Mbilinyi amewahi kuwa waziri wa Serikali ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment