Taarifa hizi nimepata hivi punde toka kwa Sillah Mbuya:
JINA LA WEBSITE: TONE INTERNET RADIO
LINK: http://www.toneinternetradio.blogspot.com
Tunapenda kuwatambulisha Watanzania wote waishio popote Duniani kwamba kuanzia sasa wanaweza sikiliza redio kupitia mtandao yani "Internet" Buree. Tumeona tufanye hivi kwa kutambua kwamba pamoja na kuwa Watanzania wengi wapo hapa nchini na wengi wao kwa sasa wanatumia Mtandao na wanapenda sikiliza redio kupitia Mtandao, lakini pia tumezingatia na Watanzania wenzetu wanaoishi nje ya nchi wapate burudani, habari na mambo mengine mengi kutoka Tanzania. Kupitia Tone Internet Radio watakuwa hawajisikii upweke na kuona kama wapo Tanzania. Pia Tone Radio inawapa nafasi wasanii wa muziki wa aina yoyote Tanzania kuleta nyimbo zao hapa studio na sisi kutangaza kazi zao bure kwa kututumia nyimbo zao kupitia toneinternentradio@yahoo.com .
Karibuni sana
Tunatanguliza shukurani zetu za dhati na karibuni sana...
Tone Internet Radio Pamoja Tutafika
Sillah Mbuya
No comments:
Post a Comment