BAADA ya kutamba na wimbo wake wa Nai Nai, msanii anaekuja juu kwa kasi na mshindi wa Tuzo mbili za Kili Music Award 2012, Omy Dimpoz, anataraji kuzindua 'single' yake mpya ya Baadae katika ukumbi wa Club Bilicanas jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu wa Kijamii, meneja wa msanii huyo, Mbaruku Issa ‘Mubenga’ alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na show itakuwa ya uhakika na ya kuvutia.
Mubenga amesema Ommy Dimpoz anataraji kuzindua wimbo huo alioufanyiwa kazi na mwandaaji wa muziki Man Water huku akkimba pamoja na mwanadada Angel.
Aidha Mubenga amesema Dimpoz atasindikizwa na wakali wa Bongo Fleva, Diamond, Ben Pol pamoja na msanii Alawi Jr pamoja na Ma DJ wakali wa Bongo kutoka kundi la Super Deejayz.
Tayari Dimpoz ameshaanza kuwasikilizisha wimbo huo baadhi ya mashabiki wake wa mikoa ya Mwanza na Moshi wakati wa Ziara ya Wakali wa Kili Music Awartd 2012 inayoendelea ambapo leo atakuwa Mbeya chini ya udhamini wa bia ya Kilimanjaro.
“Wimbo ni mkali na mashabiki wanaukubali vilivyo na tunaomba mashabiki wa Bongo Fleva make tayari kwa singo hiyo mpya itakayoanza sasa kuchezwa katika vituo vya redio na kumbi za burudani nchini kote baada ya uzinduzi huo,” alisema Mubenga.
Mubenga amewataka wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao ni mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono Dimpoz katika uzinduzi huo wa aina yake katika Klabu ya Bilicanas katikati ya jiji la Dar es Salaam Jumapili.
No comments:
Post a Comment