Timu ya waTanzania DMV imetoka sare, bila kufungana, na timu ya Ethiopia B katika mchezo uliochezwa jana huko Burtonsville, Maryland, nchini Marekani katika ligi ya Diaspora World Cup.
Kikosi kamili cha
timu ya waTanzania DMV wakiwa na mdhamini mpya wa timu hiyo, mbunifu wa mitindo
ya Kwetu, Missy Temeke, akiwa na na shabiki Didi Vava, katika uwanja wa
Greencastle, uliopo Burtonsville, Maryland.
Mchezaji wa timu ya
Ethiopia akipambana vikali na Yousouf Godson Liuzinho, kipindi cha kwanza,
katika ligi ya 2011 Diaspora World Cup kwenye kiwanja cha Greencastle, kilichopo
Burtonsville, Maryland.
Wachezaji wa wa
timu ya Ethiopia wakiwania freekick katika dakika ya 62 ya mchezo huo.
Didi Vava, kushoto,
akiwa na Sharif Qullatein, Dogo Hudhaifa Shatry, na mmiliki wa blog ya
swahilivilla Abou Shatry, wakiwa katika jukwaa la wapenzi wa timu ya waTanzania
DMV.
Mdhamini
wa timu ya waTanzania DMV ambaye ni mwanamitindo na mbunifu wa mitindo ya Kwetu
Fashion Design, Missy Temeke, akiwa na Bendera ya Taifa.
No comments:
Post a Comment