Katika mchezo wa ligi ya 2011 Diaspora World Cup unaoendelea katika viwanja
vya Hyattsville na Germantown, jijini Maryland nchini Marekani, timu ya Tanzania
DMV itachuana vikali na timu ya Ethiopia leo hii Jumamosi May 12, 2012 saa 6:00 mchana katika kiwanja cha Greencastle, kilichopo Burtonsville,
Maryland.
Kundi (B) Timu ya wa Ethiopia katika mchezo wa
awali walifungwa mabao 3-0 na timu ya Malawi ndani ya uwanja cha Greencastle,
Burtonsville, Maryland. Leo Ethiopia watajiandaa vikali ili kutaka kurudisha nguvu
zao kwa mchezo waliopoteza dhidi ya timu hiyo ya Malawi, ambayo leo itapambana na Armenia saa 7:00 mchana.
Katika mechi ya awali Armenia waliwabamiza Nigeria bao 4-1.
Tanzania DMV katika mchezo wa
kwanza siku ya Jumapili 29 April 2012 walifanikiwa kuwabamiza Ghana
mabao 3-2 ndani ya uwanja wa SoccerPlex Stadium uliyopo Ager Road Hyattsville
Maryland.
Kama kawaida yao timu ya Tanzania DMV inawaomba Watanzania wote ushirikiano wenu ili kuipa changamoto timu ya Watanzania DMV. Mnaombwa pia kufika mapema saa 5:00 kuzowea mazingira kabla ya mchezo huo kuanza.
Sehemu ya mchezo utakaochezwa leo hii ni Fairland Field 3928 Greencastle Rd. Burtonsville, Maryland 20866 Habari na http://swahilivilla.
Habari na picha kutoka http://swahilivilla.
No comments:
Post a Comment