Asasi ya HakiElimu hivi karibuni imetoa zawadi ya vitabu kadhaa kwa maktaba ya Mwalimu J.K. Nyerere iliyopo Butiama.
Maktaba ya Mwalimu J.K. Nyerere inatunza mkusanyiko wa vitabu binafsi zaidi ya 8,000 vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambavyo alivikusanya katika kipindi chote cha maisha yake, na ipo kwenye makazi yake yaliyopo kijijini Butiama.
|
Zawadi ya vitabu iliyotolewa na HakiElimu katika maktaba ya Mwalimu J.K. Nyerere, kijijini Butiama. |
Vitabu zaidi ya 50 vilivyotolewa na HakiElimu vitatunzwa kwenye maktaba hiyo, ambayo ni kivutio kimojawapo kati ya vivutio kya wageni wanaotembelea kijiji cha Butiama, sehemu alipozaliwa Mwalimu Nyerere tarehe 13 Aprili 1922, na ambapo alizikwa tarehe 23 Oktoba 1999.
No comments:
Post a Comment