Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Friday, September 14, 2012

Biashara ya vyuma chakavu na ufisidi (ni ufisidi, siyo ufisadi)

Miaka kadhaa iliyopita, mafundi toka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walijenga mnara mdogo wa kumbukumbu kijijini Butiama, sehemu ambapo ilianguka ndege ya kivita aina ya Mig, mara baada ya kuanza vita vya Kagera mwaka 1978.

Ujenzi huo uliambatana na njia ya kupita kwa miguu iliyojengewa mabomba ya chuma kuanzia barabara kuu mpaka sehemu ilipoanguka ndege, umbali wa kama mita 100 hivi.


Manara wa kumbukumbu ilipoanguka ndege ya JWTZ, eneo la Mwitongo, Butiama. Vyuma vyote vilivyo pembeni vimenyofolewa na wachuuzi wa vyuma chakavu.
Haikupita muda mrefu, wachuuzi wa biashara ya vyuma chakavu walikata mabomba yote na kuyapeleka kwa wanunuzi wa vyuma chakavu. Mnunuzi mmoja mkku wa vyuma chakavu yuko Mwanza.

Ni hawa hawa unaweza kuwasikia wakipigia makelele kuwepo kwa ufisidi (ni ufisidi, siyo ufisadi) nchini, wakinyoosha vidole kwa baadhi ya viongozi wetu, wakati hata wao wanayoyafanya hayapishani sana na yale wanayoyakemea.

2 comments:

Mija Shija Sayi said...

Tatizo ni kwamba hatuelewi nini maana kumbukumbu..au niseme wengi wetu hatujui ni kwa nini kunawekwa makumbusho, kama tungelikuwa tunajua tungeweza kuthamini mazingira ya sehemu za makumbusho hayo.

Pili..Hivi hii ndege ni kwa nini iliangukia Butiama na si kwingineko? najaribu tukujiuliza..

Madaraka said...

Baadhi ya wakazi wa Butiama wanaamini kuwa kwa sababu ilianguka pembeni ya msitu wa Muhunda, sehemu inapofanyika mitambiko ya jadi ya kabila la Wazanaki, basi iliashiria kuwa vita dhidi ya uvamizi wa majeshi ya Idi Amin tungeshinda.