Bi Victoria Gilago Bache kutoka Makumbusho ya Taifa alitembelea Butiama hivi karibuni akifanya utafiti juu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Bi Victoria ni msimamizi wa nyumba aliyoishi Mwalimu Nyerere iliyopo eneo la Magomeni, Dar es salaa, Mtaa wa Ifunda.
|
Bi Victoria akiwa ndani ya maktaba yenye mkusanyiko wa vitabu zaidi ya 8,000 vya Mwalimu Nyerere kwenye nyumba ya Mwalimu Nyerere iliyopo eneo la Mwitongo, Butiama. |
Utafiti wake ulijikita juu ya maisha ya Mwalimu na familia yake wakati wanaishi kwenye nyumba hiyo ya Magomeni kabla ya uhuru, mwaka 1961.
No comments:
Post a Comment