Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Monday, July 4, 2011

Mtanzania Mohamed Sakara aliyedhaniwa amekufa nchini Blugaria yu hai, anatafuta ndugu zake

Miezi michache iliyopita nilipokea barua pepe kutoka Bulgaria ikiniarifu kuwa kuna Mtanzania anaitwa Mohamed Sakara aliyedhaniwa amekufa lakini ilibainika kuwa yu hai na habari zake zikaandikwa kwenye gazeti moja la huko Bulgaria. 

Picha za hivi karibuni za Mohamed Sakara, akiwa jijini Sophia, nchini Bulgaria.
Raia wa Bulgaria aliyesoma hizo habari aliniandikia barua pepe kuniomba nijaribu kuwatafuta ndugu zake Sakara huku Tanzania. Nilituma hizo taarifa kwa mwanablogu Muhidini Michuzi lakini sina hakika kama zilitoka kwenye blogu yake.

Kwa kifupi Sakara alienda nchini Bulgaria kwenye miaka ya 1980 kusomea uhandisi, lakini hali ilimuendea vibaya mpaka kujikuta hana uwezo kabisa wa fedha na akiishi kwa shida mitaani. Angependa kurudi Tanzania lakini hana uwezo wa kujilipia nauli. Inasemekana baada ya kutangazwa amekufa, ndugu zake hawakuendelea kumtafuta, lakini ukweli ni kuwa yuko hai. Taarifa zake nyingine ni:
  • Amezaliwa mwaka 1961
  • Inakisiwa alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya mwaka 1982 - 1984 halafu akaenda Bulgaria ambako alikuwepo mpaka kipindi napata taarifa hizi
  • Anatoka kwenye familia ya watoto 8
  • Taarifa za kaka yake Abeid Hassan Sakara ni: amezaliwa mwaka 1954; ameandika kitabu "Jizoeze Kiswahili", na "Rashid Mfaume Kawawa"; alikuwa mkuu wa kitengo cha uchapishaji cha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (Dar es Salaam); alikuwa akiishi Upanga Mashariki, Mtaa wa Maweni, Na.244, lakini hajulikani alipo kwa sasa.
Yoyote anayemfahamu Mohamed Sakara au ndugu zake awasiliane na mimi ili nimpe anwani ya aliyenitumia taarifa hizi toka Bulgaria.

8 comments:

Subi Nukta said...

Mjomba Madaraka, ujumbe nimeusoma, nitausambaza.
Tafadhali unapopata ujumbe unaoihusu jamii, usisite kuubandika kwenye blogu yako pia hata ikiwa utawatumia wenye blogu wengine kwani wapo watu wanaoisoma blogu yako na wanaweza kuambaza ujumbe kwenye blogu nyingine, e-groups na e-forums na kusaidia kufamikisha kusudio la ujumbe.

Asante.

[Subi - wavuti.com)

Madaraka said...

Asante Subi. Nitafuata ushauri wako.

MICHUZI BLOG said...

Mdau wa Butiama,

Nami pia nimefanya kama alivyofanya Da'Subi.

Anonymous said...

Mzee Abeid Sakara namfahamu nafikiri bado yupo upanga , kwani hata Ijumaa iliopita nilimuona kwenye Msikiti wa Maamur , Upanga.
Bahati mbaya sina contact zake.

Ukweli anafanana sana na huyu ndugu.

Anonymous said...

habari,nafahamu baadhi ya ndugu zake,najaribu kuwacheck hapa, sasa watawasiliana nawe kwa njia ipi? simu labda nadhani ndo ingekuwa rahisi.

Anonymous said...

Katika tafuta tafuta yangu nimempata ndugu yake mmoja niliye happen kumjua kwa jina mmoja la Sakala nimemjulisha kwa simu namba +255655683131. Pia anasema Dr.A.Meru ni ndugu yao wameanza kulifuatilia kwa karibu.Tunawashukuru sana wapeni taarifa hao walioko huko pia.

Raymond Mkandawile said...

Ndugu nimesoma ujumbe huu na nimeguswa sana na kulingana na uzito wake basi nami nitaweka kwenye kibaraza changu ili kuwezesha ujumbe kufika kwa haraka kwa wahusika......Mungu akubariki kwa moyo huo mkuu wa kumsaidia mtanzania huyu....

Madaraka said...

Nashukuru wote kwa ushirikiano mkubwa. Anayewafahamu ndugu zake anaweza kuwapa namba yangu hii ya simu: 0755 570795. Na mimi nitajaribu kupiga hiyo simu iliyotolewa na 'Anonymous'.