Kwa mujibu wa taarifa ya Rais wa International Boxing Federation (IBF), bondia Francis Cheka ambaye alitwaa unbingwa wa mabara wa IBF wa uzito wa
middleweight tarehe 28 Aprili 2012 baada ya kumshinda bondia Mada Maugo, amevuliwa ubingwa huo baada ya kushiriki kwenye pambano ambalo halikupata idhini ya IBF.
Pambano lililomvua ubingwa Cheka ni aliloshiriki dhidi ya Karama Nyilawila tarehe 29 Septemba 2012.
|
Francis Cheka alipotwaa ubingwa wa mabara wa IBF, tarehe 28 Aprili 2012. |
Taarifa fupi ya Lindsay Tucker, ambaye ni mwenyekiti wa ubingwa wa IBF/USBA imeeleza kuwa kutokana na kanuni 5.H iwapo bingwa anashiriki katika pambano ambalo halijaidhinishwa na IBF katika uzito wake, basi ubingwa wake utatangazwa kuwa wazi pasipo kuzingatia iwapo bingwa huyo ameshinda au ameshindwa hilo pambano.
No comments:
Post a Comment