*************************************************
Ikiwa habari za siasa na hususan mkutano wa wiki ijayo wa uteuzi wa mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi kushamiri kwenye kinywa cha kila mtu mimi nageukia mada ambayo haihusiani kabisa na siasa, uendeshaji gari. Huu ni ushauri ambao unaweza kuutumia kukuwezesha kuendesha gari kwa usalama zaidi na kukuepusha na hali za kushtukiza, hasa pale unapokuwa kwenye masafa marefu.Huu siyo ushauri wa juu juu kama ule wa kukutaka ukague maji ya rejeta kabla hujaanza safari. Ni ushauri ambao pengine hutafundishwa kwenye vyuo vya udereva. Huu ushauri unatolewa na mtu ambaye ameendesha gari kwa karibia miaka 25 akiwa na ajali moja tu ndogo.
Bado sijakutana na dereva ambaye anakiri kuwa yeye ni dereva asiye wa viwango. Kwa hiyo kanuni ya kwanza ya uendeshaji gari ni: kabla hata hujawasha gari ni muhimu kujiamini; usipojiamini hakuna mtu mwingine atakayekuamini. Jichukulie kama ni mwendeshaji bora kuliko wote duniani; kile unachopungukiwa utakipata kutokana na uzoefu. Lakini usichukulie huu ushauri kwa maana yake halisi, yaani neno kwa neno kwa sababu pamoja na kuwa unajiamini bado utahitaji mafunzo ya msingi ya udereva, pamoja na kuwepo ukweli kuwa kuna watu ambao wameweza kujifunza kuendesha gari baada ya kupata leseni zao.
Kanuni ya pili ni usitoe lifti kwa watu usiowafahamu, hasa wanaume. Kuna wanaume wengi zaidi wenye makusudio ya kutenda uhalifu kuliko wanawake wenye tabia za aina hiyo. Matokeo ya tafiti ulimwenguni yanaonyesha kuwa kuna wanaume wengi zaidi wanaokutwa na hatia za jinai zaidi ya wanawake. Kwa Uingereza kwa mwaka 1984 idadi ilikuwa 86%. Kama moyo wako unakutuma kuwasaidia wenye shida nashauri utoe lifti kwa wanawake tu, lakini kuwa mwangalifu na warembo. Mara nyingine, nyuma ya mwanamke mrembo anayeomba lifti hujificha mwanaume mwenye sura mbaya mwenye nia mbaya.
Ni maoni yangu kuwa mtu ambaye ni salama kabisa kumsaidia ni mwanamke mzee. Au bora zaidi, mwanamke mwenye watoto. Yumkini kuwa hata mwanamke mwenye kusudio la kutenda kosa la jinai atawaacha watoto wake nyumbani kabla ya kujaribu kuteka nyara gari.
Siku iliyofuata tuliposikia habari za lile tukio la ujambazi tuliafikiana kuwa jambo lililonisukuma niendeshe gari kwa kasi kubwa lilituokoa kuwepo kwenye shambulio lile la ujambazi.
No comments:
Post a Comment