Naibu Waziri wa Viwanda na Bisahara, Mhe. Gregory Teu, ametembelea Butiama hivi karibuni na kutoa Shs.160,000/- kuchangia shughuli za utalii wa utamaduni zinazoratibiwa na Butiama Cultural Tourism Enterprise (BCTE).
|
Kutoka kushoto kwenda kulia: Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Gregory Teu, msaidizi wake ambaye jina lake haliweza kupatikana mara moja, na mimi, wakati nilipokuwa natoa maelezo ndani ya Maktaba ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo kwenye nyumba ya Mwalimu Nyerere aliyojengewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), eneo la Mwitongo, Butiama. |
Katika ziara yake fupi aliyofanya akiwa safarini kutoka Tarime kuelekea Mwanza, Mhe. Teu alizuru eneo la Mwitongo ambalo lenye makazi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kaburi la Mwalimu Nyerere, maktaba ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, na vivutio vingine vilivyopo Mwitongo.
No comments:
Post a Comment