![]() |
Marehemu Mariagoreth Ndangio |
Mwili wa marehemu unatarajiwa umesafirishwa leo Jumatano kuelekea Tanzania kwa ajili ya mazishi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Luton ( Luton Tanzanian Community ) Bw. John Mbwete kwa niaba ya familia ya marehemu na Jumuiya ametoa shukurani kubwa kwa watu wote waliojitoa kwa hali na mali, Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na Tanzania Association kwa ushirikiano waliotoa katika kufanikisha safari ya mwisho ya Mariagoreth kuelekea Tanzania.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, sifa na utukufu kwa Mwenyezi Mungu.
Shukrani.
*******************************
Taarifa imetolewa na:
Abraham Sangiwa
Katibu
– Luton Tanzanian Community ( TLC )
No comments:
Post a Comment