Jambo moja la msingi ambalo Watanzania tunaweza kijufunza ni kuwa maafa yaliyotokea Rwanda yanaweza kutokea pia Tanzania. Kwa mujibu wa wachunguzi wa sababu zinozogeuza binadamu mmoja kuwa adui wa binadamu mwenzake na hata kufikia hatua ya kumaliza uhai wa mwenzake ziko duniani kote.
Sababu hizi zinaanza na mchakato wenye hatua nyingi ambao hufikia mauaji kama yale yaliyotokea Rwanda. Kinachozuwia maafa kama hayo kutokea ni hatua mahususi zinazopaswa kuchukulia na jamii za kukatisha uendelezwaji wa huo mchakato.
Kwa mujibu wa Dr. Gregory Stanton wa Genocide Watch, hatua za viashiria vya kuwepo kwa mchakato na za kuzuwia maafa kama ya Rwanda ziko kumi.
Hatua ya Tano: Uratibu
Kwa kuwa mauaji ya kimbari yanaendeshwa na makundi dhidi ya makundi mengine, yanahitaji kuratibiwa. Kwa kawaida, ni dola inayoratibu maafa haya kwa kutoa fedha na silaha kwa makundi yanayoendesha mauaji.
Mfano wa Uratibu: Rwanda
Tabaka la watu wenye uwezo ndani ya Rwanda walitoa silaha kwa kundi la Interahamwe ambalo liliendesha mauaji. Serikali na wafanyabiashara wa Kihutu walitoa mapanga 500,000 na kuandaa kambi za mafunzo za "kulinda vijiji vyao" kwa kuua Watutsi.
Hatua za kuepusha Uratibu
Kuchukulia makundi yenye muelekeo wa kuchochea mauaji kama makundi ya jinai. Chukua hatua za kufanya uanachama ndani ya makundi hayo kuwa kosa la jinai na kushinikiza viongozi wao kukamatwa.
Kunyima visa kwa viongozi wa makundi haya na kukamata mali zao zilizopo nchi za nje.
Kuweka vikwazo vya silaha dhidi ya makundi yanayoeneza chuki na dhidi ya serikali zinazounga mkono chuki kwa misingi ya dini na ukabila.
![]() |
Wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 kwenye shimo hili zilikutwa maiti za maelfu ya wahanga wa mauaji hayo. |
Hatua ya Tano: Kingamizi
Katika hatua hii mambo kadhaa yanajitokea, ikiwa ni pamoja na :
- wenye siasa kali wanakuwa na nia ya kutenganisha makundi
- makundi yenye kuchochea chuki na kuchapisha propaganda yenye nia ya kugawa watu
- sheria zinapitishwa kuharamisha ndoa kati ya watu na makundi yanayokusudiwa kuwa tofauti
- wenye msimamo wa kati wananyamazishwa, kutishwa, na kuuwawa
Mifano ya Kingamizi: Ujerumani
Maandamano yaliandaliwa dhidi ya wafanyabiashara wenye asili ya Kiyahudi, na Wajerumani wenye msimamo wa kati waliopinga kitendo hiki ndiyo walikamatwa kwanza na kupeleka kwenye kambi za mauaji.
Hatua za kuepusha Kingamizi
Pinga kwa kila hali sheria na sera zinazobagua makundi au zinazonyima haki za kiraia kwa makundi. Weka walinzi wa silaha kulinda viongozi wenye msimamo wa kati, kama ambavyo imefanyika Burundi. Shinikiza kuachiliwa kwa viongozi wenye msimamo wa kati ambao wanakamatwa, na kudai na kuendesha uchunguzi kwa wale viongozi wa aina hiyo ambao wameuwawa.
Pinga kupinduliwa kwa serikali na makundi yenye siasa kali.
Itaendelea na:
- Hatua ya Saba: Mipango
- Hatua ya Nane: Mateso
Taarifa nyingine zinazohusiana na hii:
http://muhunda.blogspot.com/2013/11/hatua-kumi-za-mauaji-ya-kimbari-3-na-4.html
http://muhunda.blogspot.com/2013/11/hatua-kumi-za-mauaji-ya-kimbari-3-na-4.html
No comments:
Post a Comment