Katika mpambano wa marudiano kati ya Rashidi Matumla na Maneno Oswald uliyofanyika tarehe 25 Februari 2012 katika ukumbi wa PTA Dar es Salaam, Matumla alimshinda Oswald kwa pointi.
|
Rashidi Matunla (kushoto) akimaliza ubishi kati yake na Maneno Oswald (kulia) katika pambano lao la tarehe 25 Februari 2012. |
Katika pambano hilo la raundi 10 katika uzito wa "Super Middleweight" matokeo ya waamuzi yalikuwa kama ifuatavyo: Anthony Ruta 97 - 93; Pemba Ndava 95 - 95; na Ramadhani Basta 97 - 95.
Kwa matokeo haya Matumla ameshinda mapambano matatu kati yao na kutoka sare
pambano moja, wakati Maneno ameshinda pambano moja na kutoka sare moja.
No comments:
Post a Comment