Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Friday, December 28, 2012

Lugha yetu Kiswahili: Kamusi ya Kiswahili kwenye mtandao

Hivi karibuni nililazimika kutafuta maana ya Kiswahili ya neno la Kiingereza dilemma na tafsiri iliyopo kwenye Kamusi ya Kiingereza - Kiswahili iliyochapishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tole la 2006, imetoa neno "mtanziko."

Lakini TUKI hao hao kwenye Kamusi yao ya Kiswahili - Kiingereza, toleo la 2001, hawajatoa maana ya neno hilo kwa lugha ya Kiingereza. Inawezekana kuna toleo lijalo ambalo litaweka maana ya "mtanziko" kwa lugha ya Kiingereza.
Hali kadhalika toleo la mwaka 2004 la Kamusi ya Kiswahili Sanifu iliyochapishwa na Oxford University Press nalo halina neno hilo.

Nilifanya utafiti kidogo kwenye mtandao na kugundua wavuti inayoitwa The Kamusi Project ambayo inayo kamusi ya Kiingereza - Kiswahili - Kiingereza inayoruhusu watumiaji kutafuta maana ya maneno na inaruhusu pia hata mtumiaji kuongeza maneno ambayo hayapo kwenye kamusi hiyo. Nyongeza ya maneno hupitiwa na mtaalamu na inapoonekana ni sahihi basi inaorodheshwa rasmi kwa matumizi na watumiaji wengine.

2 comments:

Martin Benjamin said...

Asante sana, tazama hapa: http://kamusi.org/node/259757

Karibu sana kuchangia kwenye Kamusi! Lakini "definition" ya neno la Kiswahili ni maana yake KWA KISWAHILI. Kwa maana yake kwa Kiingereza, ni lazima kuchagua "Translation".

(Bado hatujapata nafasi kuweka maelezo ya tovuti kwa Kiswahili, kuna kazi mno...)

Madaraka said...

Asante, tunaendelea kujifunza.