TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
JANUARY
6, 2012
Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa Afrika (IBF/Africa) limemteua Bw. Miraji Mrisho Kikwete
kuwa Makamu wa Rais anayeshughulikia maendeleo ya vijana katika bara la Afrika,
Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati. Uteuzi wa Miraji unaanza January mwaka
mpya 2013.
Katika
kumteua Miraji, Rais wa IBF katika bara
la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Bw. Onesmo Ngowi alisema kuwa Miraji ana uwezo wa
kuwahamasisha na kuwaunganisha vijana katika shughuli za maendeleo.
Aliendelea
kusema kuwa Miraji atakuwa anawahamasisha vijana, kuwaunganisha, kuwajengea
uwezo wa kimaendeleo yatakayoratibiwa na IBF.
Aidha, Rais
huyo alisema kuwa Miraji atakuwa anabuni njia mbalimbali za kuwaunganisha
vijana wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ili waweze kufaidika na
miradi ya IBF ambayo inalenga kwenye elimu, kujenga vipaji pamoja na
kuwaunganisha kwenye biashara ya utalii wa michezo.
Katika
mkutano wake wa mwaka uliofanyika katika jiji la Honolulu, jimbo la Hawaii,
nchini Marekani hivi karibuni IBF iliupokea mradi wa “Utalii wa Michezo” uliobuniwa na kuwakilishwa na Rais wa IBF
katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtazania Onesmo
Ngowi.
Lengo kuu
la mradi huo ni kulifanya bara la Afrika, hususan Tanzania, kuwa kitovu kikuu cha
“Utalii Michezo” hivyo kujenga
uchumi imara. Nchi za Tanzania na Ghana ziliteuliwa kuwa nchi za mfano kwenye
mradi huo.
Katika
mradi huo, IBF itatumia mtandao ilionao katika nchi zaidi ya 203 duniani
kuhamasisha wanachama wake na famlia zao, wapenzi pamoja na marafiki zao kuja
Afrika/Tanzania kutalii pamoja na kuwekeza katika miradi mbalimbali.
Uteuzi wa
Miraji utasaidia kuwaunganisha vijana ili waweze kuchangia na kufaidika na
biashara ya utalii kwenye mradi huo na umefanywa wakati muafaka.
Miraji
ambaye ni mjasiriamali amejipambanua katika maendeleo ya jamii na ana mchango
mkubwa sana katika kuendeleza vijana nchini Tanzania.
Rais Ngowi
alimwelezea Miraji kama tegemeo ambalo vijana wanalihitaji kwani wanahitaji
uhamasishaji wa hali ya juu na Miraji ana uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa
ufanisi mkubwa kwani alishawahi kuifanya kwa kipindi kirefu.
Miraji
Mrisho Kikwete ni msomi wa Chuo Kikuu cha nchini Oman ambako amesomea elimu ya
utawala wa biashara ambayo ndiyo lengo kuu la uteuzi wake. Ana haiba ya
kupendwa na vijana pamoja na uwezo wa kujichanganya nao.
Imetolewa
na:
Makao makuu
IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati
Dar-Es-Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment