****************************************************
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUFAFANUA KUHUSU MIRADI YA
UTAFUTAJI NA UVUNAJI WA GESI ASILIA NCHINI
1.0 UTANGULIZI
Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa ufafanuzi wa miradi ya Gesi Asilia ambayo itatekelezwa kwa kushirikiana na wawekezaji katika Sekta
ndogo ya Gesi Asilia na kueleza manufaa makubwa yatakayopatikana kwa wananchi
wote wa Tanzania wakiwemo wale wa Mikoa ya Mtwara na
Lindi.
Siku
ya Alhamisi, tarehe 27 Disemba 2012, baadhi ya Vyama vya Siasa
vya Upinzani viliratibu na kuhamasisha baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara, wengi wao wakitokea Mtwara Mjini kufanya
maandamano ya kudai raslimali ya Gesi Asilia iwanufaishe wakazi wa Mtwara na kupinga mradi mkubwa wa ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia kutoka Mtwara hadi
Dar
es Salaam. Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa taarifa
ifuatayo kwa Wa-Tanzania wote kwa kupitia
vyombo vya habari.
Tokea
Uhuru, uchumi wa Tanzania umetegemea kilimo cha mazao ya
biashara kama vile katani (Tanga na Morogoro), pamba (Mwanza, Mara
na Shinyanga), kahawa (Kilimanjaro, Kagera, Ruvuma na Mara), chai (Iringa) na tumbaku (Tabora). Fedha za mazao haya zimewanufaisha
wakazi wa mikoa yote ya nchi yetu bila ubaguzi wo wote wala wakulima
wa kutoka mikoa hiyo hawajawahi kufanya maandamano wakidai
upendeleo (dhidi ya Wa-Tanzania wengine)
wa aina yo yote ile.
1
Mapato yatokanayo na uchimbaji wa dhahabu (Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga na Tabora), almasi (Shinyanga) na tanzanite (Manyara) yamewanufaisha Wa-Tanzania wote bila ubaguzi wo wote ule! Minofu ya samaki wa Ziwa Victoria (Mara, Mwanza na
Kagera) imeliingizia Taifa letu fedha nyingi ambazo zimetumiwa na wakazi wa nchi nzima bila ubaguzi
wo wote.
Aidha kuna mikoa ambayo inazalisha mazao ya chakula kwa wingi kwa
manufaa ya Wa-Tanzania wote. Mahindi kutoka Rukwa, Mbeya, Ruvuma na Iringa
yanasafirishwa kwenda mikoa yote ya nchi yetu bila kujali eneo
yanakolimwa na wakazi wa mikoa hiyo hawajawahi kudai mahindi hayo
ni kwa ajili
ya watu wa mikoa hiyo pekee. Sukari ya Kilombero, Mtibwa
na Kagera inatumiwa na wakazi wa mikoa yetu yote bila ya kuwepo madai ya mikoa inayozalisha sukari hii kupewa upendeleo wa
aina yo yote ile. Maji ya Mto Ruvu yanatumiwa na wakazi wa Dar Es Salaam bila
manung’uniko yo yote kutoka kwa wakazi wa eneo la chanzo cha Mto Ruvu.
Umeme wa kutoka Mtera, Kidatu na Kihansi (Dodoma na Morogoro),
Hale (Tanga), na Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro) unatumiwa na wakazi wote wa Tanzania bila ubaguzi au malalamiko ya
wenyeji
wa sehemu ambazo umeme huo unafuliwa na kusafirishwa kwenye Gridi ya Taifa.
Kwa
hiyo, kutokana na mifano hii michache, ni wajibu wa wazalendo na
wapenda maendeleo wa kweli na hasa Wa-Tanzania wanaopinga ubaguzi
wa aina yo yote ile kujiuliza kwa kina sababu zilizopelekea Vyama Siasa
vya Upinzani kupanga, kuhamasisha, kushabikia na kuongoza
maandamano ya tarehe 27 Disemba
2012 pale Mtwara
Mjini.
2.0 RASLIMALI YA GESI
ASILIA TANZANIA
Gesi
Asilia ilianza kugundulika hapa nchini tangu mwaka 1974 kwenye Kisiwa
cha
Songo Songo, Mkoani Lindi.
Baada ya hapo
Gesi
Asilia imegundulika maeneo ya Mtwara Vijijini, yaani
Mnazi Bay (1982) na Ntorya (2012), Mkuranga (Pwani, 2007), Kiliwani (Lindi, 2008). Kiasi cha
Gesi Asilia iliyogunduliwa katika maeneo haya inakadiriwa kuwa Futi za
2
Ujazo Trilioni 4.5 – 8.
Katika
kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na kasi kubwa ya utafutaji
Mafuta na Gesi Asilia uliojikita
zaidi kwenye maji
ya
kina
kirefu
cha
bahari. Kiasi cha Gesi
Asilia
iliyogundulika katika kina kirefu cha maji inafikia
takribani Futi za
Ujazo Trilioni 27. Kiasi cha wingi wa Gesi Asilia yote iliyogunduliwa
nchi kavu na baharini inafikia
takribani
Futi
za Ujazo Trilioni 35.
Kufuatana na Sheria
za
nchi yetu
zinazotumiwa
kugawa mipaka ya mikoa iliyopo kando
kando mwa bahari (isivuke 12 nautical miles au
22.22 km kuingia baharini), Gesi Asilia iliyogunduliwa hadi sasa katika
Mkoa wa Mtwara pekee ni asilimia 14 tu ya gesi yote iliyogundulika
nchini. Kwa kutumia
kigezo hicho cha Sheria za
mipaka ya
ki-utawala ya
mikoa yetu, Lindi inayo
7% ya gesi yote, Pwani
1% na huku Kina Kirefu cha Bahari (Deep Sea) ndicho chenye gesi nyingi (78%) kuliko mikoa
yote ikiwekwa pamoja! Kwa hiyo, hakukuwa na haja ya kufanya maandamano kwa sababu Gesi Asilia nyingi inapatikana kwenye bahari
ya kina kirefu ambayo iko
ndani ya mipaka ya nchi yetu bila kujali
mipaka ya mikoa yetu. Isitoshe Gesi Asilia imegundiliwa kwenye miamba
tabaka (sedimentary rocks) yenye umri wa Miaka kati ya Milioni 199.6
hadi 23.03. Mipaka ya Bara la Afrika, ya nchi yetu na ile ya mikoa yetu
haikuwepo
wakati huo!
Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia pia unaendelea tukiwa wa mategemeo
makubwa ya
upatikanaji
wa
raslimali
hizi katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Manyara, Kigoma, Mbeya, Njombe,
Rukwa, Katavi,
Morogoro na Tabora pamoja na kwenye kina kirefu cha maji baharini kuanzia mpaka wetu na Msumbiji hadi mpaka wetu na Kenya. Hatutarajii mikoa hii nayo ifanye maandamano ya kutaka
kuhodhi
raslimali za Gesi Asilia na
Mafuta zitakapogunduliwa
mikoani
mwao.
3.0 MATUMIZI YA GESI ASILIA YA MNAZI BAY (MTWARA) NA
SONGO SONGO (LINDI)
Mpaka hivi sasa Gesi Asilia inayozalishwa na kutumika nchini ni kutoka
Mnazi Bay (Mtwara Vijijini) na Songo Songo (Kilwa, Lindi). Gesi ya Mnazi
3
Bay
kwa sasa huzalisha umeme kwa ajili ya Mikoa ya Mtwara na Lindi
tu. Mitambo ya kufua
umeme kutokana na Gesi Asilia iliyopo Mtwara Mjini inao uwezo wa kuzalisha MW 18 lakini
matumizi
ya umeme ya
Mikoa ya Mtwara na Lindi haijavuka MW 12. Umeme huo wa Mtwara
unafuliwa na TANESCO huku Kampuni za Wentworth na Maurel & Prom
zikizalisha Gesi Asilia (inayotumiwa na TANESCO) kiasi cha Futi za Ujazo Milioni 2 kwa siku. Ikumbukwe kwamba ufuaji wa umeme wa hapo Mtwara Mjini ulikuwa mikononi mwa Kampuni ya Artumas iliyofilisika. Tangu Desemba 2006 hadi leo hii kiasi cha gesi kilichotumika kufua umeme kwa ajili ya mikoa hiyo miwili ni chini ya asilimia 1 ya gesi yote iliyogundulika Mnazi Bay (Mtwara Vijijini).
Vilevile ikumbukwe kwamba kuna
visima
vinne vya Gesi
Asilia
pale Mnazi Bay (Mtwara Vijijini) na kinachotumika kwa sasa na tena kwa
kiwango cha chini kabisa ni kimoja tu!
Aidha ni vizuri
ndugu zangu Wa-Tanzania wakaelewa kuwa Gesi Asilia hii inatafutwa na kuchimbwa na wawekezaji wenye
mitaji mikubwa,
wataalamu na teknolojia ya utafutaji na uchimbaji wa Gesi Asilia ambao wanapaswa kurejesha mitaji yao. Uchorangaji wa kisima kimoja cha
utafutaji wa Gesi Asilia nchi kavu unahitaji Dola za Marekani Milioni
40, na kwenye kina kirefu cha maji baharini zinahitajika zaidi ya Dola za Marekani Milioni 100. Ikumbukwe kwamba, Serikali kwa
kushirikiana na Shirika la Mafuta la Tanzania (TPDC), inatumia fedha za
walipa kodi wa nchi nzima kwa shughuli za kuvutia, kuratibu na
kusimamia utafutaji na uendelezaji wa Gesi Asilia nchini kote ikiwemo
Mikoa ya Mtwara na Lindi. Walipa kodi Wa-Tanzania bado hawajalalamika wala hawajafanya maandamano ya kudai fedha zao za kodi
zisitumike huko
Mtwara!
Ni muhimu pia tukaelewa kwamba Gesi Asilia iliyopo Mnazi Bay (Mtwara Vijijini) inazalisha umeme
peke yake kwa ajili ya Mikoa ya Mtwara na Lindi. Gesi Asilia ya Songo Songo (Kilwa, Lindi) ndiyo inayotumika kuzalisha umeme kwa ajili ya Gridi ya Taifa, na pia kwa ajili ya
wananchi wa Kisiwa
cha
Songo Songo (Lindi),
maeneo ya Somanga
4
Fungu (Lindi) na viwandani (Dar Es Salaam). Tangu Oktoba 2004 ambapo mitambo ya kufua umeme ilipoanza kazi hadi leo hii, kiasi cha Gesi Asilia ya Songo Songo kilichotumika ni asilimia 7 tu ya Gesi Asilia yote iliyogunduliwa huko. Kwa hiyo, takwimu zinaonyesha kwamba hata
uchumi wa Jiji la Dar Es Salaam unatumia kiasi kidogo sana cha Gesi
Asilia (7%) iliyopo Songo
Songo
(Kilwa,
Lindi).
Ikumbukwe kwamba
waajiriwa kwenye viwanda vya Dar Es Salaam wamo wanyeji wa kutoka
Mtwara Mjini ambako maandamano yalifanyika na vilevile wamo
wafanyakazi ambao ni wanachama wa Vyama vya Siasa
vya Upinzani vilivyopanga, ratibu na kushabikia maandamano ya Mtwara Mjini ya tarehe
27
Disemba 2012.
4.0 MIPANGO YA MATUMIZI YA GESI ASILIA KATIKA KIPINDI CHA
MIAKA 5 HADI 10
(a) Ujenzi wa
Bomba
la Gesi Asilia hadi Dar Es Salaam:
Kuuza Gesi Asilia Jijini Dar es Salaam, kitovu cha uchumi wa
Tanzania (80% ya mapato ya nchi yetu yanazalishwa Dar Es Salaam) ni uamuzi mzuri wa ki-uchumi. Tayari kuna viwanda
34 vinatumia Gesi Asilia
ambavyo vinahitaji kupanua shughuli zao endapo gesi zaidi
itapatikana. Soko kubwa la Gesi Asilia
lipo tayari Dar es Salaam (na siyo Mtwara), ambapo ipo
mitambo ya kufua umeme kwa kutumia mafuta. Serikali
inatumia fedha nyingi za kigeni kununulia mafuta ya kufua
umeme tunaoutumia kila siku. Takribani Dola za Marekani Bilioni Moja (sawa na Shilingi Trilioni 1.6) kwa mwaka
zitaokolewa kutokana na mitambo iliyopo nchini ikifua umeme
kwa
kutumia Gesi Asilia na kuachana na mafuta ambayo ni ya
bei
kubwa sana.
Bei
ya
umeme kwa
uniti
moja (KWh)
ya
umeme unaofuliwa kutumia dizeli na mafuta ya aina nyingine ni kati ya Senti za Marekani 30 hadi 45 na huku bei ya uniti
moja
hiyo hiyo ni Senti za Marekani 6-8 kwa umeme utokanao na Gesi Asilia na
zinapungua na
wakati wa matumizi.
Vilevile, takribani Dola za Marekani millioni 202 kwa mwaka zitaokolewa iwapo Jiji la Dar Es Salaam litatumia Gesi Asilia badala ya mafuta katika magari, taasisi na majumbani. Fedha
5
hizi zikiokolewa zitatoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa
Taifa letu kwa manufaa ya Wa-Tanzania wote wakiwemo wale waliondamana na wale walioratibu maandamo ya Mtwara Mjini ya tarehe
27
Disemba 2012.
(b) Umeme mwingi
zaidi
kutokana na
Gesi Asilia:
Bomba la Gesi Asilia linalojengwa litasafirisha gesi nyingi zaidi
ambayo itawezesha mitambo mipya itakayojengwa Kinyerezi (Dar
Es Salaam) kufua
umeme wa zaidi ya MW
990.
Umeme mwingine utafulia Somanga Fungu
(Lindi) wa kiasi
kisichopungua
MW
520.
(c) Usafirishaji na
usambazaji wa
umeme nchini mwetu:
Dar es Salaam ndiko kuna miundombinu mikubwa ya
usafirishaji na
usambazaji wa umeme
kuliko mikoa mingine
yote, hivyo ni uamuzi wa ki-uchumi unaotulazimisha kusafirisha Gesi Asilia kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara na kuipeleka Dar Es Salaam ambako itatumika kufua umeme, na kutumika moja kwa
moja
viwandani, majumbani na
kwenye magari.
(d) Kwa
kuzingatia mahitaji
ya Gesi
Asilia yatakayojitokeza:
Bomba la kusafirisha gesi litawekewa matoleo ya kuchukulia gesi
(tie-off) katika maeneo ya Mtwara, Lindi, Kilwa na Mkuranga
ili kuhakikisha kuwa miji hii inakuwa na Gesi Asilia ya uhakika
wakati wowote itakapohitajika. Kwa hiyo kuweka mitandao ya
usambazaji wa gesi kutoka kwenye Bomba la Gesi Asilia
linalojengwa kutarahisisha
matumizi ya Gesi Asilia viwandani na
majumbani katika Mikoa ya Mtwara na Lindi, na kwenye mikoa mingine kwa siku za
baadae.
(e)Serikali imetenga maeneo katika pwani ya Mikoa ya Kusini
(Lindi na Mtwara) kwa ajili ya uanzishwaji wa maeneo ya
viwanda (Industrial Parks/Estates) vikiwemo viwanda vya
mbolea, Liquefied Natural Gas (LNG) na Petrochemicals. Ujenzi wa kiwanja cha sementi uko katika hatua za mwisho za
maandalizi.
(f) Ili kutengeneza mazingira mazuri ya biashara ya Gesi Asilia na
Mafuta kwa kampuni za huduma, malighafi na vitendea kazi,
Serikali imetenga eneo maalumu Mtwara,
ambalo
litawekewa
6
miundombinu ya msingi ili kutoa vivutio mbalimbali kwa
makampuni hayo. Eneo hilo litapewa hadhi ya Ukanda Huru wa
Bandari (Freeport Zone).
Ni
lazima shughuli za kusafisha na kusafirisha Gesi Asilia zitatoa ajira
katika
maeneo
husika. Kwa
mfano kwa
mitambo ya
kusafishia
gesi
inayojengwa Madimba (Mtwara Vijijini) na SongoSongo (Kilwa, Lindi), kila mtambo utahitaji wafanyakazi na wengine watatoka Mikoa ya Lindi na
Mtwara.
Watanzania wanakumbushwa kuwa
raslimali zilizopo nchini ikiwemo
gesi asilia, madini, makaa ya mawe, wanyama pori, misitu, milima ya
utalii, mito, maziwa, bahari n.k ni za Wa-Tanzania wote kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Raslimali hizi
zinapatikana, zinatunzwa na kuzalishwa maeneo mbalimbali nchini
mwetu na mapato yake yanatumika kwa maendeleo ya Wa-Tanzania wote
bila
kujali maeneo raslimali
hizo zilipo.
Tusikubali kuvunja nchi yetu vipande vipade kwa kisingizio cha raslimali zilizopo mikoani
mwetu. Tusikubali kuvunjavunja mikoa yetu kwa kisingizio cha raslimali zilipo kwenye wilaya zetu.
Tusikubali kuvunjavunja wilaya zetu kwa kisingizio cha raslimali
zilizopo kwenye tarafa zetu. Tusikubali kuvunjavunja tarafa zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye kata zetu. Tusikubali
kuvunjavunja kata zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye
vijiji vyetu na
mitaa
yetu.
MUNGU
IBARIKI TANZANIA, DUMISHA UHURU NA UMOJA WETU
Prof Dr Sospeter Muhongo (Mb)
WAZIRI YA NISHATI NA MADINI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
7
No comments:
Post a Comment